Posts

Showing posts from 2015

HIVI NDIVYO UNAVYOWEZA KUPOTEZA MUDA WAKO

Habari zenu rafiki zangu natumaini hamjambo na mnaendelea vizuri kiafya. Leo tutazungumzia kuhusu muda na jinsi unavyoweza kuupoteza hata kukukatisha tamaa ya kuendelea kupambana kama tulivyokubaliana kwamba kila tutakachojifunza ni lazima  tuangalie suala la afya zetu linahusika kwa kiasi gani kuathiri utafutaji wetu na kutugubika kwenye wimbi la umaskini na kujikuta tunakata tamaa . Katika suala la utafutaji utafiti unaonesha asilimia nyingi za watu waliokata tamaa na kusitisha juhudi zao za kuhakikisha wanafikia mafanikio yao zinachangiwa na maradhi ambayo huwahitaji watumie muda mwingi kujitibia au kutafuta fedha za matibabu ambazo Mara nyingi humfanya mtafutaji ambaye ni mgonjwa mwenyewe kusimama au kwa mtafutaji muuguzaji kushindwa kupanga mambo yake uzuri na badala yake kujikuta kila anachopata kuishia kwenye  matibabu na kujikuta anakata tamaa ya kupambana kufikia ndoto zake.zifuatazo ni njia mbadala zitakazo kusaidia kukabiliana na changamoto kama hii hata kabla hujakumbana na