HIVI NDIVYO UNAVYOWEZA KUPOTEZA MUDA WAKO

Habari zenu rafiki zangu natumaini hamjambo na mnaendelea vizuri kiafya. Leo tutazungumzia kuhusu muda na jinsi unavyoweza kuupoteza hata kukukatisha tamaa ya kuendelea kupambana kama tulivyokubaliana kwamba kila tutakachojifunza ni lazima  tuangalie suala la afya zetu linahusika kwa kiasi gani kuathiri utafutaji wetu na kutugubika kwenye wimbi la umaskini na kujikuta tunakata tamaa . Katika suala la utafutaji utafiti unaonesha asilimia nyingi za watu waliokata tamaa na kusitisha juhudi zao za kuhakikisha wanafikia mafanikio yao zinachangiwa na maradhi ambayo huwahitaji watumie muda mwingi kujitibia au kutafuta fedha za matibabu ambazo Mara nyingi humfanya mtafutaji ambaye ni mgonjwa mwenyewe kusimama au kwa mtafutaji muuguzaji kushindwa kupanga mambo yake uzuri na badala yake kujikuta kila anachopata kuishia kwenye  matibabu na kujikuta anakata tamaa ya kupambana kufikia ndoto zake.zifuatazo ni njia mbadala zitakazo kusaidia kukabiliana na changamoto kama hii hata kabla hujakumbana nayo.

1.jifunze kuishi kwa kufuata kanuni za afya.
     Kuna mambo mengi ya kiafya ambayo wengi wetu hatuyatilii maanani kana  kwamba si mambo ya kuzingatiwa.
Mambo hayo ni
      (a)kunawa kwa maji safi na sabuni kabla na baada ya kula.
      (b)kunawa kwa maji safi na sabuni baada ya kujisaidia na kujikausha vizuri.
      (c)kunywa maji safi na salama au yaliyochemshwa na kuchujwa vizuri .
      (d)kula kwa wakati wakati wote .
kuosha matunda kabla ya kumenya na kula.
      (e)Kujijengea tabia ya kupima afya zetu mara kwa mara(full body checkup).
Hizi ni baadhi ya kanuni za afya ambazo wengi wetu tumezichukulia poa na kutozifuata mara kwa mara inapotubidi  kufanya hivyo .

2.fanya mazoezi ya viungo mara kwa mara ,usikubali kubweteka ukauruhusu mwili wako kuzoea hali ya kutochangamka ,hali ya kuwa dhaifu ,hii hupelekea hata kudumaa kwa akili,uzito wa kufanya maamuzi na uvivu wa kufikiria .hakikisha unapata japo nusu saa ya kufanya mazoezi kwa afya ya mwili wako kila siku ni muhimu ipe ulazima.

3.Upe mwili wako muda wa kupumzika kuna watu wamekuwa wagonjwa kwakutopumzisha miili yao.zoea kupenda kubadili mkao pia...usikae zaidi ya masaa mawili bila kujinyoosha na kubadili mkao ili kupumzisha viungo vya mwili wako.wapo wengi wanaumwa mgongo kwa sababu hawakuwa na tabia ya kubadili mkao katika kazi zao.
hakikisha hukosi muda wa kupumzisha mwili wako kwa kupata usingizi wa kutosha pia kubadili mikao.

imeandikwa na Antony Mwakilima.
Mawasiliano:  0756 351 462
                            0672 314 874
email:     mwaijox@gmail.com

         KWA PAMOJA TUNAWEZA

Comments

  1. Hii ipo poa nimeipenda Sana shukrani kwa ushauri wako.

    ReplyDelete

Post a Comment

Popular posts from this blog

AVUMILIAYE MPAKA MWISHO NDIYE ATAKAYEOKOKA!

KIPIMO UNACHOPIMIA WENGINE NDICHO UTAKACHOPIMIWA

HASIRA HASARA