HADITHI YA KUKU

Habari ya leo rafiki yangu, siku yako imekaaje? Natumaini tuko pamoja na tunaendelea kujifunza pamoja karibu tena tujifunze kupitia kisa cha kuku.

Jifunze kutoka kwa kuku ....
Ninayo hadithi fupi ya kweli ambayo imetokana na kitu nilichojifunza kwa kuku mmoja nikiwa ninalima shamba. Unajua unapotambua kuwa kuku na wao wanakula ndipo unapojua kuwa nawao wanatafuta ulaji(ridhiki)!

Sasa basi kulikuwa na kuku watatu wawili matemba na mmoja jogoo. Miongoni mwa matemba alikuepo temba mmoja mdogo, huyu ndiye aliyenisukuma nikuhadithie habari hizi.
Huyu kuku alikuwa anatafuta chakula chake na haikuwa tu chakula lakini ni wadudu ambao huwa ni adamu kipindi cha kiangazi na mbaya zaidi wanaishi ndani ya ardhi. Ni wadudu fulani jamii ya funza weupe wanapendwa sana na kuku! Mambo niliyoyaona kwa kuku huyo,

1) Huyu kuku alijua anachokiataka. Licha ya kuzungukwa na kuku wengine wakubwa bado hakuwa muoga, hakuwaogopa kuku wenzie cha ajabu kabisa hata mimi na jembe hakutuogopa alichokiangalia ni kupata hao wadudu tu.

Funzo; Kama kuku huyu aliweza kusimamia anachokitaka mpaka akipate bila kujali mazingira basi sisi ni zaidi maana tunaoutashi, twaweza kujiuliza kabla ya kuamua. Kikubwa ni kujua unachokitaka ,ukijua unachokitafuta huwezi kuyumbishwa na pia itakuwa na mikakati imara ya kuhakikisha unakipata.

2) Kuku huyu alijitambua.Kwa vile alikuwa mdogo alitambua akizubaa hatapata kitu hivyo alikuwa makin sana kuhakikisha kila nikitoa jembe baada ya kulima anakimbilia kuokota hao wadudu.

Funzo; Wakati huu vijana tunanguvu za kutosha ndio wakati pekee tunaweza kukimbizana na fursa mbalimbali za kimaisha, tunapaswa tujitambue kwamba tukiendelea kusubiri mazingira yafaayo hatuwezi kupata tunayoyataka kwani umri haurudi nyuma na ukishazeeka hutaweza kuwa mwepesi tena kama ilivyokuwa kwa hao kuku wakubwa walikuwa hawawezi kukimbia kwa kasi kama huyo mdogo hivyo kila walipofika yule mdogo alikuwa ashakula wadudu wengi.

3) Aliyajua mazingaira yake yamezungukwa na maadui wake alihakikisha anatazama vizuri kabisa kiasi kwamba kuna wadudu kuku wenzake na mimi mlimaji hatukuwaona yeye aliwaona.

FUNZO; Kuna watu wengi sana wamekuwa wakihoji mazingira ya kazi watakazozifanya mfano kwa waajiriwa wengi, hawajaiona fursa itokanayo na mazingira wanayoyaona si rafiki kwao na kazi zao utasikia kule kijijini mno hakuna hata Huduma za jamii mimi huko siendi au nitahama.
Kwa wajasiliamali matatizo na changamoto ni fursa za kuwapeleka kwenye ndoto zao, hebu jiulize hapo unapoishi na kupaona ni mjini au kuna Huduma zote za jamii palianza hivyo au palikuwaje kabla? Je si mtu mmoja mwenye viungo sawa nawewe alianza kupabadilisha?
Ama hakika tukijua tunachokitaka kuna fursa tutaziona ambazo wengine hawazioni katika mazingira hayohayo usiruhusu mazingira yaathiri ndoto zako badala yake tumia mazingira kuziona fursa zaidi za kukupeleka kwenye ndoto hizo.

4) Hakuchoka. Alichonifurahisha zaidi nikwamba hakukubali kuchoka kutafuta hata walipoanza kumdonoa kuku wenzake bado alikimbilia sehemu ambayo kulikuwa na ndugu yangu akilima pia.

FUNZO; Huyu kuku nilivutiwa naye nikaendelea kumfuatilia nikagundua hakukubali kupoteza muda kuhangaika na  adui zake alichokifanya alikuwa anahama mazingira akiona amedonolewa huku anahamia kule. Yawezekana kuna biashara unafanya lakini unakutana na watu wengi wanaoiga na kufanya kama wewe acha kushughurika nao boresha Huduma zako kwa kuongeza thamani ya bidhaa zako au uangalie sehemu nzuri ambayo unaweza kuendelea kufanya biashara yako hiyohiyo kwa mafanikio zaidi! Usipoteze muda kuanza kushughurika na washindani wako angalia wanafanyaje badili mtazamo Fanya tofauti kidogo tu utaona mabadiliko.
Usitishwe na washindani wako.

5) Hakukata tamaa wakati wote.Kwa kuwa hakukata tamaa, akaonekana anafaidi sana sasa kuku wote wakaanza kumfuata wanamuangalia anaenda wapi wanamfuata hatimaye na wao wakaanza kuambulia japo kidogokidogo.

FUNZO; 1) Ukijua unachokitaka ukaweka juhudi kukipata pasipo kukatishwa na kukata tamaa utakuwa mfano mzuri na wakuigwa kwa wengine kwa hiyo usiangalie wengine wanafanya nini nawewe ufanye bali wewe fuata kanuni za kupata unachotaka watakuja wenyewe na utakuwa msaada wao.

             2) Kuna hatua utafikia kwenye maisha yako huwezi kuvuka peke yako angalia wenye ndoto kama zako walivukaje hapo Fanya nawewe utaanza kuona matunda kidogokidogo" wenye ndoto kubwa hawazifikii peke yao" .

Ahsante kwa kuwa pamoja nami katika Kisa hiki ninaamini umejifunza kitu.

Je, wewe ungewaona kuku hao ungejifunza nini?

Imeandikwa na Antony Mwakilima.
Mawasiliano:     0756 351 462
                             0672 314 874
email:     mwaijox@gmail.com      

       TAFAKARI BADILI MTAZAMO
                         ©2017

Comments

Popular posts from this blog

AVUMILIAYE MPAKA MWISHO NDIYE ATAKAYEOKOKA!

KIPIMO UNACHOPIMIA WENGINE NDICHO UTAKACHOPIMIWA

HASIRA HASARA