UNAPOKUWA MWANAMKE!

Habari ya wakati huu wapendwa wasomaji wa makala zetu. Nikupe hongera kwa kuendelea kuweka muda wako kwa ajili yetu ili tujifunze pamoja.
Karibu tusherehekee kwa namna hii siku hii ya leo ambapo mama zetu,wapenzi wetu,rafiki zetu wa kike na ndugu zetu wanaadhimisha siku yao.

Unayonafasi kubwa sana Duniani,kuna vitu vingi sana vinanisukuma kusema hivi mfano pasipo mwanamke isingekuwa rahisi Yesu kuja duniani kama mwanadamu,haijalishi mimba ilitungwaje tunachojua alikuja duniani kupitia mwanamke,sijui ni wanawake wangapi wanaiona hii nafasi kubwa kabisa waliyopewa na MUNGU,kulibeba kusudi kubwa la wokovu wa wengi.Upande mwingine Mwanamke ndiye mtunza familia ndiye anayejua nani yuko wapi anafanya nini wakati gani,Kitu ambacho mwanaume huelezwa tu kama taarifa anaejua kipi kimepungua kipi kinahitajika nyumbani, hela si tatizo, tatizo ni Jana tulikula hiki na Leo tule kile husimamia yeye.Anategemewa na familia, amefanywa kuwa msaidizi wa mwanaume yaani uwepo wake ni kumfanya mwanaume aweze anaposhindwa,maana anayemsaidia mwingine ni mwenye uwezo zaidi ya anayesaidiwa kwamba mwanaume akikwama asimame yeye kumsaidia mpaka atoke alipokwama, Sijui kama wanawake wanaitambua nafasi hii kubwa pia waliyopewa, Lakini nataka kusema kama mwanamke atasimama kwenye nafasi yake basi hakuna jambo litakaloharibika, hakuna ndoa zitakazovunjika hovyo, hakuna familia zitakazoteseka hovyo. Hakutakuwa na migogoro makanisani.Kule kujiona hawawezi, kule kujiona hawana sauti, kule kusema" mimi ni mwanamke tu nitabaki mwanamke" kumewafanya wamepoteza nafasi zao kwenye familia,kanisa,jamii na taifa kwa ujumla. Kama Mungu alikuamini kwamba utalibeba kusudi lake kwa miezi tisa na akakupa kumsaidia mwanaume pia, kwa nini usijiamini?

Hebu chukua hatua sasa usimame kwenye nafasi yako,utambue uwezo mkubwa Mungu aliokupa kama Mwanamke ukamsaidie mwanaume kulibeba kusudi la Mungu na kulitimiza,Hebu jiulize ungesimama kwenye nafasi yako ungekuwa hivyo ulivyo? Familia, kanisa, jamii na taifa lako lingekuwa hapo?Na kama sivyo unafanya nini hata Leo kukaa kwenye nafasi yako? Unasubiri nini kumpa Mungu utukufu kwa kukupa nafasi kubwa namna hiyo?

Ewe mwanamke itambue nafasi yako ujenge familia,kanisa,jamii na taifa lako!!!

HERI YA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI!

Imeandikwa na Antony Mwakilima.
Mawasiliano:     0756 351 462
                             0672 314 874
email:     mwaijox@gmail.com      

       TAFAKARI BADILI MTAZAMO
                         ©2017

Comments

Popular posts from this blog

AVUMILIAYE MPAKA MWISHO NDIYE ATAKAYEOKOKA!

KIPIMO UNACHOPIMIA WENGINE NDICHO UTAKACHOPIMIWA

HASIRA HASARA