KIONDOE HICHO KIUNGO

Natamani kuzungumza na mtu mmoja saa hii.
Habari yako ndugu, jamaa na rafiki yangu?
Naamini u mzima wa afya njema na unaendelea kukaza buti ukifanya juhudi kufikia mafanikio ya ndoto zako.

Karibu tena ndugu, leo tatazungumzia habari ya kuondoa au kung'oa au kutoa kiungo kwamishi. Kiungo kinacholeta vikwazo kwa safari tuliyonayo ya mafanikio.

Kuna Kitu ambacho usipokijua kitakusumbua sana kitakufanya wakati mwingine uishi maisha ya utumwa na unapokuja kushituka unakuta tayari mambo yamekwisha haribika na huna tena muda wa kuishi maisha yakwako.
Imeandikwa ukiona kiungo chochote cha mwili wako kinakukosesha king'oe, kiondoe au kitoe kisiwe sehemu yako kwa sababu ni heri ukose kiungo kimoja uende uzimani kuliko kuwa na viungo vyote jehanamu. Ni kitu gani basi kitakachokupa wewe maumivu makubwa namna hii zaidi ya mwili wako? Kama ni hivyo mbona unataka kufanikiwa lakini umeendelea kukumbatia marafiki wanaokukwamisha? Hao marafiki ulionao mbona hawakusaidii kuishi maisha uliyokusudiwa? Mbona unaishi maisha yao? Umekuwa mtumwa wao. Nataka nikwambie ukiendelea kuwakumbatia hautaishi maisha yako wala kuzifikia ndoto zako, waondoe wasiwe sehemu yako maana wanakwamisha mafanikio yako. Kadiri unavyowang'ang'ania kwa kigezo cha kutoka mbali, au watakuonaje ndivyo unavyopoteza muda wa kuishi maisha yako. Nasemaje piga chini hao wanaokurudisha hatua tatu nyuma ukipiga hatua moja mbele. Wakatae Aliyekupa kusudi ndani yako atakuletea marafiki ambao ni sawa yako, Marafiki watakaokubeba kuelekea mafanikio yako, furaha yako.
USIKUBALI KUYAKOSA MAONO ULIYONAYO KWA SABABU YA VIUNGO VYAKO MWENYEWE. Marafiki wasiofaa ni viungo vyakuondoa ni heri ubaki na kiungo kimoja uishi maisha yako kuliko ukawa na viungo mia ukawa mtumwa wa maisha yao.
Kumbuka kuna uhusiano mkubwa sana kati ya mafanikio yako na viungo vyako yaani marafiki unaoshirikiana nao. Kama huwezi kujisimamia watakupoteza, Chukua tahadhali Fanya maamuzi sahihi!!!

Imeandikwa na Antony Mwakilima.
Mawasiliano:     0756 351 462
                             0672 314 874
email:     mwaijox@gmail.com      

       TAFAKARI BADILI MTAZAMO
                         ©2017

Comments

Popular posts from this blog

AVUMILIAYE MPAKA MWISHO NDIYE ATAKAYEOKOKA!

KIPIMO UNACHOPIMIA WENGINE NDICHO UTAKACHOPIMIWA

USIMDHARAU MTU YEYOTE