CONNECTION

Habri rafiki zangu? Nafurahi kwa sababu natambua tuko pamoja na tunaendelea kunufaika na vitu ambavyo Mungu hutufundisha juu ya maisha yetu ili tuweze kusonga mbele hata kufikia yale maisha ameyakusudia kwetu. Karibu tena tushirikishane kuhusu Connection.

Napenda kusema neno kidogo kuhusu connection(muunganiko au uhusiano), unajua watu wote tunapenda mambo mazuri yatokee kwenye maisha yetu. Kuna wakati tumekutana na fursa mbalimbali tumeshindwa kwa sababu tunapenda mambo mazuri tu bila connection.
Napozungumzia connection namaanisha uhusiano kati ya hicho unachokipenda na upatikanaji wake. Nitakupa mfano wengi wetu tumezoea kutumia maneno yafuatayo, ninayaweza yote kwake yeye anitiaye nguvu... Amesema tutashinda na zaidi ya kuahinda, atatufanya kichwa na si mkia n.k zipo nukuu nyingi tu ambazo tumekuwa tukitembea nazo. Sasa nataka ujiulize tangu umeanza kutembea na hizi nukuu umeona tofauti? kwanini unashindwa? Kwanini huwi kichwa?

Ukiwa mwanafunzi hakuna Kitu kinatiliwa mkazo uwapo kwenye chumba cha mtihani kama kufuata maelekezo. Kwa hiyo unaweza ukauona mtihani ni mwepesi kabisa lakini suala la kufaulu linabaki kwenye maelekezo inamaana kufuata maelekezo kunampa mwanafunzi connection kati yake na ufaulu anaoutaka. Angalia ambao hawakufuata maelekezo walipata matokeo gani! Ukiambiwa uandike jibu katika desimali usipofanya hivyo huwezi kupata. Ukiambiwa uandika sentensi katika wakati uliopita ukaandika uliopo hupati Kitu kwa sababu ufaulu wako upo kwenye maelekezo tu! Sasa kwa MUNGU ni zaidi. Ukitaka kuwa kichwa lazima usikie sauti na utii. Maanake katika kusikia sauti kuna maelekezo(connection) ambayo ukitii unakuwa kichwa. Iko wazi kabisa kila unalolitaka liwe kwenye maisha yako Lina taratibu zake ambazo ukizifuata linakuwa. Utashinda na zaidi ya kushinda, je kweli unapambana au umekaa tu unasubiri ushindi uje? Unayaweza yote kwake yeye akutiaye nguvu, je ni kweli uhusiano wako na yeye unamruhusu kukutia nguvu ya kuyaweza yote?
Tambua kila unachokitaka kinamaelekezo ya jinsi ya kukipata, tafuta maelekezo kabla hujaanza kukitafuta. Wengi wetu tunaangalia na kutaka mambo mazuri tu bila kufuata maelekezo ndio maana hatuwi tunavyotaka tuwe na hatupati tunavyopaswa! Mungu akusaidie uone uhusiano uliopo kati ya unachokitaka na jinsi gani utakipata.

Imeandikwa na Antony Mwakilima.
Mawasiliano:     0756 351 462
                             0672 314 874
email:     mwaijox@gmail.com      

       TAFAKARI BADILI MTAZAMO
                         ©2017

Comments

Popular posts from this blog

AVUMILIAYE MPAKA MWISHO NDIYE ATAKAYEOKOKA!

KIPIMO UNACHOPIMIA WENGINE NDICHO UTAKACHOPIMIWA

USIMDHARAU MTU YEYOTE