FANYA UNACHOKIPENDA

Habari ya leo tena mpendwa msomaji na rafiki yangu ?ni matumaini yangu kuwa uko na afya njema kabisa inayoimarika kila siku kwa ajili ya kukuwezesha kuweka bidii zaidi hata kufikia mafanikio uyatakayo.


Ni vema sana kuupa mwili wako kile unataka kwa ajili ya kuwa na afya njema ,nguvu na kukupa ujasiri wa kupambana mpaka umeona mafanikio au umepata kile unachotaka.


Fanya unachopenda mwenyewe. Nasisitiza tena fanya unachokipenda wewe mwenyewe.Hapa nazungumzia habari ya kufanya chochote halali chenye matokeo chanya kwenye maisha yako na yanayokuzunguka,kuna mambo mengi mazuri unatamani kuyafanya kutoka moyoni mwako lakini pengine umekutana na wanaokupinga usifanye au wanaokuzuia kufanya hicho kisichoharamu unachopenda kufanya.
kwa nini ufanye unachokipenda?


Kufanya unachokipenda itakufanya


1/uweke bidii kubwa tofauti na yule anayefanya kitu asichokipenda au anayeshinikizwa kufanya jambo asilolipenda.
Ndio wengi wameshindwa kutimiza ndoto zao au maono yao ya kimaisha kutokana na kufanya mambo wasiyoyapenda licha ya kuyaweza lakini wamejikuta wanashindwa kuweka bidii au kufanya juhudi kwa kuwa hawakuwa tayari kufanya mambo hayo,licha ya kuwa wakati mwingine unaweza kuweka bidii lakini ni rahisi kukata tamaa inapotokea ugumu wowote,mfano mwanafunzi anaesomea fani anayoipenda baba au mama yake,ni kweli atasoma atafanikiwa lakini atakuwa ameua ndoto zake au malengo au maono yake kitu ambacho kinaweza kumchukulia muda mwingi sana kuyakaribia mafanikio aliyoyataka au kutoyafikia kabisa.


2/Utamani kuona kile unachokipenda kinafanikiwa.
Licha ya ugumu,changamoto na matokeo ya kukukatisha tamaa bado unapata nguvu ya kuendelea kufanya zaidi ili kuthibitisha kwamba ni kitu unachokipenda na haukubali kushindwa kirahisirahisi ,na kwamba una maono nacho.


3/Uamini kwamba unaweza bila kujali walioshindwa.
Ndio ukipenda kitu hauwi tayari kukiacha japo wengine  wamekiacha,hata kama wanaofanya kitu hicho kama wewe wanashindwa unaamini uwezo binafsi na ule utofauti wenu unatosha kukutia moyo kuendelea kufanya bila kukata tamaa.


4/Uongeze ufanisi katika utendaji wako.
Unapofanya kitu unachokipenda unafanya kwa ufanisi mkubwa maana unataka wengine wajue kwa nini unakipenda ,unakuwa tayari kujifunza zaidi ili ufanye kilicho bora chenye kuongeza thamani kwa wengine.Unatafuta ueledi zaidi kila wakati ukifanye kionekane bora.
mfano,wagunduzi wa kompyuta pakato(laptop)walianza na kompyuta nyumba, kompyuta za mezani wakaendelea kutafuta ueledi wa kuboresha zaidi na kutengeneza laptop.


5/Utake kuthibitisha uzuri au ubora wa jambo unalolifanya kwa wengine.
Licha ya kuwepo kwa maneno yasemayo hakilipi unachokifanya au hakina faida bado unaiona faida na malipo makubwa sana na unaongeza nguvu ya kufanya zaidi ili uthibitishe kuwa malipo /faida huanza pale unapoamua kufanya unachokipenda na sio kwa kushauriwa au kushinikizwa kufanya. Unaona thamani na fursa ambazo wengine hawazioni kwa kile unachokipenda,mfano;unapenda kuigiza lakini unaambiwa uigizaji bongo ,umekosa kazi za kufanya?Lakini kwa kuwa ndicho ukipendacho hukatishwi tamaa na maneno ya watu badala yake unataka uwe muigizaji mkubwa Duniani ili uthibitishe thamani ya kile ukipendacho.


6/Uwe na furaha hata kama bado hujafikia kilele cha mafanikio utakayo.
Ile kwamba unafanya unachokipenda moyo wako na roho yako vinaridhika basi unakuwa mtu wa furaha hata kama bado hujaona matunda lakini kufanya jambo vizuri ni kulifanya kwa furaha.Ukitaka kujiona mwenye furaha maishani mwako anza kufanya mambo unayoyapenda usikubali kuyumbishwa na mtu yeyote, mfano wa kufanya usichokipenda ni sawa na kuoana na mke/mume usiyempenda sio rahisi kufurahia maisha ya ndoa na pia si rahisi kuwa hata na wasaa wa kujadili mustakabali wa maisha yenu, kwa kifupi sio rahisi kushirikiana kwa pamoja kutimiza azima ya ndoa na ndoto za kila mmoja wenu!
Tambua unachotaka, fanya unachopenda, ishi kwa furaha.


Imeandikwa na Antony Mwakilima.
mawasiliano: 0756-351 462
                          0672-314 874
email: mwaijox@gmail.com


                    ©2016


Comments

Popular posts from this blog

AVUMILIAYE MPAKA MWISHO NDIYE ATAKAYEOKOKA!

KIPIMO UNACHOPIMIA WENGINE NDICHO UTAKACHOPIMIWA

HASIRA HASARA