ACHA KUTAMANI KUWA KAMA MWINGINE.

Habari ya wasaa huu rafiki zangu naimani nyote hamjambo na mnaendelea kuyafanyia kazi tunayojifunza kila wakati,nataka tujifunze kuhusu saikolojia ya kutammani kuwa kama mtu fulani au mtu mwingine,saikolojia hii ni kwamba hutafanya cha kwako ila cha yule unaetamani kuwa kama yeye.


Ndio ni muhimu sana kulitambua hili usitamani kuwa kama mimi na mimi nisitamani kuwa kama wewe kwa sababu ifuatayo ,kama mimi nikitamani kuwa kama wewe ,je ni nani atakayefanya kile Mungu amekusudia kifanyike kupitia mimi?pia kama wewe ukitamani kuwa kama mimi nani basi atakayefanya kile ambacho Mungu ametaka kifanyike duniani kupitia wewe?.Hii ndio sababu muhimu ya kukwambia usitake kuwa kama yeyote yule kwa kuwa hakuna kama wewe mwingine yaani wewe au mimi ni watofauti sana ukilinganisha na mwingine,na huo utoafauti wetu ndio thamani yetu.Kile kitu kinachokutofautisha na mimi ndio kitu kinachoutambulisha ubora wako ,thamani yako, uwezo wako na yamkini upekee ulionao.


Kila mtu duniani amepewa kitu cha kufanya tofauti kabisa na alichopewa mwingine ,ile kwamba sote ni waimbaji si tija lakini ule utofauti wa viwango vya uimbaji ndio haswa thamani inayokutofautisha na mwingine,huyu akiimba besi mwingine sauti ya kwanza na yule ya pili akawepo mwingine sauti ya tatu apo tunapata timu ya waimbaji ,wa sauti ya kwanza kwelikweli akitamani kuimba sauti ya nne  tutakosa sauti ya kwanza na tutaharibu timu yetu.Tatizo sio ualimu lakini kile kiwango cha ufundishaji ambacho huteka fahamu za wanafunzi na kuachilia uelewa wa mambo mbalimbali wanayofundishwa ndio unaomtofautisha mwalimu mmoja na mwingine .Si lazima tupishane mambo tunayoyafanya yanaweza kuwa sawa ila yakatofautiana ubora na viwango kiutendaji.Jiulize kama mkono ungetamani kuwa kama mguu ni nani angeshika?kama jicho lingetamani kusikia ni nini kingetazama au kuona?kama ulimi ungetamani kunusa kama ifanyavyo pua ni nini kingeonja ladha?


Najua licha ya kuwa na kitu cha thamani kubwa ndani yako bado umetamani kuwa kama mwingine.Yawezekana hujafahamu ni kipi ulichopewa kufanya na thamani yake ndio maana umekubali kutamani na kufanya juhudi ili kuwa kama mtu fulani na sio kuitoa thamani iliyowekwa ndani yako ambayo kuna kundi kubwa la watu limekuwa likisubiri uitoe iwasaidie kutoka hatua fulani ya maisha hatimae kufikia mafanikio.Ndio kuna watu wanaishi maisha hayo waliyonayo kwa sababu wewe hujafanya cha kwako lakini pia yawezekana kama ungefanya cha kwako ungeweza kupiga hatua zaidi ya hii uliyopo sasa.


Unapoona vitu mfano vikombe,majumba ,vyombo vya moto n.k vimetengenezwa na watu ambao hawakutamani kuwa kama wengine badala yake walifanya mawazo ambayo ndio thamani yenyewe waliyopewa yawekwe kwenye matendo na hatimae tukawa na vitu hivyo.Usikubali kuishi maisha ya wengine kutokana na kutamani kuonekana kama wao ,kutamani kuwa kama mwingine ni sawa na mkono kusema namimi nataka kutembea kama mguu,unaitia timu udhaifu kwa kuikosa thamani yako kwa kutamani na kufanya yale yanayofanywa na wengine pia.Dunia haipaswi kubaki ilivyo panapo uwepo wako,inakungoja wewe ufanye cha kwako ibadilike!!!


imeandikwa na ANTONY MWAKILIMA.
Mawasiliano; 0756 351 462
                    0672 314 874
email:mwaijox@gmail.com


Comments

Popular posts from this blog

AVUMILIAYE MPAKA MWISHO NDIYE ATAKAYEOKOKA!

KIPIMO UNACHOPIMIA WENGINE NDICHO UTAKACHOPIMIWA

HASIRA HASARA