ATHARI HASI KUTOKANA NA WATU WAKO WA KARIBU

Natumaini kuwa hujambo na unaendelea vizuri na mapambano ya maisha kuhakikisha unapata unachotaka. Nashukuru Mungu
ni siku nyingine njema ambayo tunaendelea kujifunza juu ya mambo ambayo hutusaidia kufikia vilele vya mafanikio tunayoyataka.

                      


Ndio kuna athari nyingi hasi ambazo zimetokana na ndugu zetu,rafiki zetu,wapenzi wetu ,wazazi wetu pia ambazo zimechangia kuwa na maisha tuliyonayo sasa aidha kwa ushawishi wao kwako juu ya kile wanachokiamini au kwa shinikizo kutoka kwao ufanye kipendacho roho zao. Wapo ambao wamekushurutisha au kukulazimisha na kukushinikiza kufanya jambo ambalo moyo wako haukuwa tayari wala wewe binafsi hukulipenda lakini kwa heshima yao ukafanya ili waridhike bila kujua kwamba kufanya kitu usichopenda ambapo unakuwa hauko tayari, hauna amani na hufurahii kufanya kunapunguza ufanisi, ubunifu na ueledi wako kwa jambo ulipendalo.


Kuna watu wameolewa kwa kulazimisha aidha kutokana na umasikini au tamaa za wazazi wao,wengine wameachana na wenzi wao ambao walipendana sana na kuwa na miadi mingi juu ya kesho yao kwa sababu,wazazi hawakupendezwa na mmoja kati yao aidha kwa dini,kabila au utajiri na hivyo kupelekea watoto wao kukutana na watu wasiosahihi kwenye maisha yao ambao wameharibu ndoto zao na malengo yao ya kimaisha hususani mafanikio.
kwa kuwa katika ndoa mke hubeba urithi wa mume ndio maana tunasisitizwa kuwa makini kabla ya kuoa ili tusijekukosea kuoa mke mwenye urithi wa mwanaume mwingine na kuvuruga mpango wa Mungu juu ya yale aliyotupa kufanya kwenye maisha yetu.


Wengine wakiwa katika mahusiano wamedanganywa na wapenzi wao wakapata mimba na baada ya kuzaa wakatelekezwa na kukatishwa kwa ndoto zao kukafikia hapo.


Wengine yawezekana wameshauriwa na ndugu zao au watu wao wa karibu kwa habari ya utajiri wa masharti ili wawe na mafanikio makubwa kwa muda mfupi na bila kutumia nguvu nyingi wakaweka imani zao pembeni wakakubali kutoa ndugu zao ,wazazi wao sadaka ili wawe matajiri wakubwa lakini hatima yake wameishia kupata laana na kuishi maisha ambayo hawakutarajia mfano hawajazifaidi mali zao aidha wamechanganyikiwa na kupoteza malengo yao kabisa.


Yawezekana kwa namna yoyote ile marafiki uliowaamini ukawaeleza habari zako mipango na malengo yako wamekuwa ndio watu wenye nia ya kukukatisha tamaa na kukurudisha nyuma. Wamekuwa watu wakukupa sababu na mifano mingi ya walioshindwa ili kuzuia usiendelee kutimiza ndoto za maisha yako na hivyo kukujengea uoga wa kuthubutu.


Unaweza ukawa umegundua ni kwa kiasi gani watu wa karibu wanaweza kuwa wameathiri maisha yako hata mbali na mifano hii. Kuna watu ambao kila ukitaka kufanya jambo wamekuwa wakishauri acha,ni gumu,wengi wameshindwa,utapata hasara,hutafika popote na ukifanya hivyo huwezi kufika mbali n.k, Na wewe umekubali  hofu yao iamue juu ya maisha yako kwa kuwa umewapa umuhimu na kuwaamini.
Naomba nikuekeze kidogo,Usikubali kuwapa nafasi watu wengine waamue hatima ya maisha yako amini maisha yako na ndoto zako ziko mikononi mwako usiruhusu hofu ya unaowaamini iamue utakachokifanya. Lazima tujifunze kujitegemea kimawazo licha ya kupokea ushauri kwa wengine.


Wengi wameua ndoto zao na malengo yao kwa kushirikiana,kukubaliana,kushawishiwa,kushinikizwa au kudanganywa na watu wanaowaamini kuwa hawawezi kuwaharibia maisha ,ni dhahiri kwamba hatukatai kupokea ushauri lakini ushauri haupaswi kuwa maamuzi ya mwisho ya maisha yako.Wengine wameacha hata kusikiliza dhamiri zao kutokana na mashauri ya watu wengine.
Waswahili wakasema ukipewa  changanya na yako pata kitu kamili ingia kwenye vitendo bado, hujachelewa anza sasa kuboresha maisha yako!!!


imeandikwa na Antony Mwakilima
mawasiliano:    0756 351 462
                         0672 314 874
email: mwaijox@gmail.com


         
          KWA PAMOJA TUNAWEZA
                           ©2016

Comments

Popular posts from this blog

AVUMILIAYE MPAKA MWISHO NDIYE ATAKAYEOKOKA!

KIPIMO UNACHOPIMIA WENGINE NDICHO UTAKACHOPIMIWA

HASIRA HASARA