HASIRA HASARA

Habari za leo rafiki yangu!bila shaka uko vizuri na unapiga hatua kila unaporuhusu ubongo wako upokee vitu vipya na kukuongezea thamani katika maisha yako.


Leo ni siku nyingine tena tunayofuraha kuungana pamoja kujifunza kuhusu hasira hasara ,hebu jiulize ni mara ngapi umeruhusu hasira iamue juu ya hatima ya maisha yako licha ya kuijua methali hii? unadhani maamuzi uliyochukua ukiwa na hasira yamekuwa chanya kwenye maisha yako? kama hasira imekupa athari hasi za maamuzi uliyochukua ukiwa umeudhiwa ,umechukua hatua gani hata sasa?


Naomba upate muda utafakari kiasi ambacho maisha yako yameathiriwa kutokana na maamuzi uliyofanya ukiwa na hasira, hebu mtazame Kaini alichofanya baada ya kutawaliwa na hasira alimuua nduguye Abeli, na baada ya hapo akaingia kwenye laana ambayo hakika ilisababisha maisha yake yasiende vizuri. Yawezekana kabisa alijua kwamba akiua ndugu yake mambo yake yatakuwa mazuri na pengine atakubalika badala yake kampoteza ndugu na laana juu.


Je,ni mara ngapi umesikia habari za watu kuchomana visu na kujeruhiana au kuuana kabisa kwa sababu aidha wamesalitiwa au kufumania wenzi wao?


Je,hujawahi kuona au kusikia watu wakiharibu na kuvunja mali zao, vyombo au vifaa vyao vya ndani mfano simu,tv,redio,vyombo vya chakula,chupa za chai n.k kutokana na hasira zao halafu zinapoisha wanaanza kujuta na kujilaumu kwa maamuzi waliyoyachukua kwa kuwaingizia hasara?


Je,hujasikia habari ya mtu kujidhuru mfano,Baada ya kumfumania mkewe akitoka nje ya ndoa kwa kuwa mumewe hakutahiriwa na alipoulizwa hakusita kusema hivyo na mume kuona amedharirishwa kwa watu kwamba hajatahiriwa  akaamua kujikata sehemu zake za siri licha ya kuwa na mke aliyemsisitiza juu ya tohara.je,kujikata kumesaidia kuondoa tatizo la kuchepuka kwa mkewe?


Bila shaka habari hizi unazisikia kila leo,ndio hutokea kila mara kwa sababu watu wengi hawajui jinsi ya kuziongoza na kuzizuia hasira zao kabla hawajafanya maamuzi. Uwapo na hasira si rahisi kufanya maamuzi ya busara kwa maisha yako na wenzako.
Hasira haikupi muda wa kufikiria matokeo ya maamuzi yako
1. kama yatakuwa hasi au chanya 2.kama yatatatua tatizo au       
    kuliongeza
3.kama yatakurejeshea furaha au  
    kuiondoa kabisa
4.kama utafarijika na kuwa na   
   amani au ndio utaingia mazingira 
   ya msongo zaidi amani itoweke
   kabisa?


Siku zote hasira humuongoza mtu kufanya mabaya ,jifunze hapa jinsi ya kuzuia hasira!


Kabla hujafanya maamuzi yoyote ni lazima ujiulize matokeo kwanza ya kile utakachokiamua,je kitaathiri vipi maisha ya kwako na wengine?
kamwe usiruhusu hasira iamue juu ya maisha yako kwa sababu hasira ni hasara!


Imeandikwa na Antony Mwakilima.
mawasiliano: 0756-351 462
                         0672-314 874
email: mwaijox@gmail.com


                    ©2016


Comments

Popular posts from this blog

AVUMILIAYE MPAKA MWISHO NDIYE ATAKAYEOKOKA!

KIPIMO UNACHOPIMIA WENGINE NDICHO UTAKACHOPIMIWA