USIMDHARAU MTU YEYOTE

Habari yako mpenzi msomaji wetu?Bila shaka u mzima wa afya.Ni wakati mwingine tena siku nyingine tukiwa na hamasa nyingine nakukaribisha tuungane pamoja kujifunza juu ya usimdharau MTU yeyote!

USIMDHARAU MTU
Ndio natumaini kila mmoja wetu kama binadamu yawezekana kabisa kuna mazingira umekutana nayo kwenye maisha ukawadharau wengine au kuna Hadhi umepata ikakupelekea uone wewe pekee ndio unamaana na umuhimu.Nataka nikuambie usimdharau mtu awayeyote kwa sababu,

Bado hujajua kila Kitu
Yawezekana kwa hilo ulifanyalo wapo wenye maarifa zaidi ukiwadharau hutayapata.usijione kwamba huwezi tena kuhitaji maarifa yoyote kutoka kwa wengine, ni muhimu sana kujua hili ikiwa unataka kufanikiwa ni lazima uwe mchezaji mzuri wa timu yako ,maarifa yetu yanatofautiana na uwezo wa kufanya mambo vilevile kwa hiyo badala ya kudharauliana,golikipa anapaswa asimdharau mfungaji wake ama beki ili waweze kushirikiana vizuri hebu tushikane mikono kama timu tucheze pamoja ndivyo wengine wanavyofunga magoli na kuibuka washindi.

Bado hujaweza kila Kitu
Hakuna binadamu anayeweza kufanya kila Kitu kwa hiyo ni lazima tutambue kuwa udhaifu wa mtu mmoja unakamilishwa na mtu mwingine ,hivyo ambapo wewe ni dhaifu yupo ambae si dhaifu eneo hilo ila ni dhaifu kwingine na wewe ndiye wakumsaidia pia kinyume chake ni kwamba hapo penye udhaifu wako asiyedhaifu eneo hill ndio msaada wako,ukimdharau labda kwa hadhi aliyonayo utapoteza mtu wa kukusaidia kupiga hatua Fulani kimaisha kutokana na ule udhaifu ulionao eneo Fulani.Usiangalie jinsi ulivyo ukajiona unaweza kila Kitu, la tunategemeana hivyo usidhani elimu yako,cheo chako au hadhi yako inatosha kukufanya uwadharau wengine,kwa kufanya hivyo wengi wamebaki palepale hawasongi mbele maana wanadhani wanaweza kila Kitu na hivyo hawataki kujua wengine wanafanyaje wawasaidie kwa sababu wamejiona wanaweza kila Kitu wakawadharau.

Bado humjui mtu atakayetumiwa na MUNGU Kwa ajili yako.
Kwa kuwa MUNGU si mwili Bali ni roho hutusaidia kimwili na kiroho kupitia wanadamu.kwa sababu hiyo hakuna anayefahamu ni nani asimdharau kwa kuwa atatumika kumvusha hatua Fulani kwenye maisha yake au ni nani amdharau kwa kuwa hatohusika kwenye maisha yake.
Kutokana na sababu hiyo hupaswi kumdharau yeyote kwenye maisha yako ili yule aliyekusudiwa asije akaghairi kutenda impasavyo kama mjumbe wa MUNGU kwako kwa sababu ya dharau zako

Bado huijui kesho yako
Ndio ni kweli hakuna anayejua kesho atakuwa wapi, akifanya nini, na nani ?kwa huijui kesho yako inakupasa uwe mnyenyekevu sana kwa MUNGU wako ili akupe hekima ya kuweza kujua jinsi ya kuishi na watu hapa duniani.Naam ili uishi vizuri na wengine unahitaji kuwa na hekima, kuna watu unaweza kuwaona ni bure kabisa au ukawaona hawana lolote au ukawaona hawana mbele wala nyuma ukawadharau. Je unaijua kesho yako itakuwaje? Bila shaka hujui hivyo basi, unapaswa utambue kuwa hadhi uliyonayo,cheo au elimu vitaendelea kuwa na thamani kesho kutokana na unavyoishi leo. Pengine kesho ukaishiwa au kufilisika sasa jiulize kama uliyemdharau wakati huu uko vizuri akawa ndiye mtu pekee wa kukusaidia utaweza kumuomba msaada?sawa, unaweza ukajitosa ukajaribu lakini je,unahakika atakusaidia?vipi kama ungeishi nae kwa hekima au ungemuheshimu vivyo alivyo?isingekuwa rahisi kukusaidia?

Sasa basi kwa kuwa hujui kesho yako itakuwaje usimdharau mtu maana mali,vyeo au hadhi na elimu ni vya kupita tu ila binadamu mwenzio unapomthamini 
na kumuheshimu unajijengea hazina ya kesho yako. Inawezekana upo hapo ulipo kwa sababu ya dharau zako kwa wengine,
MUNGU akusaidie sana ili uache kudharau wengine nawe ujiwekee hazina ya kudumu kwenye maisha yako.

Imeandikwa na Antony Mwakilima.
Mawasiliano:     0756 351 462
                            0672 314 874
email:     mwaijox@gmail.com

       TAFAKARI BADILI MTAZAMO
                           ©2017

Comments

Popular posts from this blog

AVUMILIAYE MPAKA MWISHO NDIYE ATAKAYEOKOKA!

KIPIMO UNACHOPIMIA WENGINE NDICHO UTAKACHOPIMIWA

HASIRA HASARA