SIKU YA FURAHA NI LEO

Ninayofuraha siku nyingine tena kushirikiana ujumbe huu pamoja nawe mpenzi msomaji wa makala katika blog yetu,sina shaka unaafya njema na unaendelea kuweka bidii kwa ajili ya kuifikia safari ya mafanikio tuyatakayo!


Ndio siku ya furaha ni leo!
Tunapaswa kuiishi leo kana kwamba ni siku ya mwisho,tukiishi kwa furaha! Lazima usahau kuhusu jana ndipo unaweza kuishi leo vizuri na kwa furaha kwa sababu,


Jana imekuwa ni siku ya kuumiza kwako,umeumizwa kwa mambo mengi mfano mahusiano, dhuluma, magonjwa, kuonewa, kushindwa na kukatishwa tamaa, kukataliwa n.k


Jana imekuwa ni siku ya huzuni sana kwako,umehuzunishwa na misiba ya watu waliokuwa msaada wako wa karibu, unafiki wa marafiki na wale uliowaamini, ugumu wa maisha, utawala wa rushwa n.k


Jana imekuwa ni siku ilijaza moyo wako uchungu kutokana na mateso ya mama wa kambo, ndugu wenye roho mbaya, kuibiwa na kunyang'anywa haki, kunyanyasika kutokana na hali ya umaskini,kupanda kwa gharama za maisha n.k


Kuna wakati kutokana na jana ikivyokuwa watu wengine hawakutamani wafike leo! wapo ambao wamajirahisi,wamejiua wamejinyonga,wamewajeruhi waliowasababishia jana yao kuwa na majeraha yenye maumivu makubwa mioyoni mwao jana.
Hakika jana haipaswi ikumbukwe maana kuikumbuka jana ni kurudusha maumivu,unyonge,huzuni na uchungu ambao utakunyima kuifurahia leo yako na kuweza kuitumia kwa faida!
kutokana na jana wapo wameweka kisasi mioyoni mwao,wapo wamewabeba wale waliowakosea mioyoni mwao,pasipo kujua kwa kufanya hivyo kila leo yao imekuwa kama jana ya maumivu na majeraha makubwa!


Njia pekee ya kuisahau jana yako na kuweza kuitumia leo vizuri kwa mafanikio yako ni hii hapa;


SAMEHE NA KUSAHAU JANA YAKO
Ukisamaehe na kusahau kabisa unayohakika ya kuifurahia leo yako,ukisamehe unajihisi wepesi moyoni mwako unakuwa ni mwenye amani na hujutii jana yako tena na kuiona leo kuwa ni siku ya ushindi kwako.


USIWE MTU WA KISASI
Ukitaka kufanikiwa leo jifunze kuchukulia udhaifu wa wenzio na kusonga mbele kwa sababu kulipiza kisasi ni sawa na kujiingizia udhaifu uleule wa mwenzio wewe mwenyewe na hivyo kufanya wewe na yeye kukosa tofauti na hii roho ya kisasi ukiiruhusu siku zote itakutaka ulipize kisasi hata kwa jambo dogo!


USIWEKE KINYONGO MOYONI MWAKO
Unapokuwa umembeba mtu moyoni ile kusema sitasahau alichonifanyia fulani, ipo siku tu na yeye atanikuta ngoja mambo yakae vizuri...nimemsamehe sitamsahau inamaana bado unaumizwa na kile alichofanya jifunze kuwaachilia watu moyoni mwako ndipo furaha na amani ya leo huja!


Siku ya furaha ni leo usikubali kuishi pasi na furaha siku ya leo kwa maana mafanikio huja uwapo na furaha ambapo moyo wako na akili zako vina uhuru wa kuyatafakari maisha yako na kupanga mikakati ya kupiga hatua zaidi ,badala ya kuwaza jinsi ya kuwakomesha ,kuwalipiza kisasi na kuwaumiza waliokuumiza,kukujeruhi na kukuhuzunisha jana.
Wasamehe na uwaachilie ufurahi leo kwa ajili ya mafanikio yako ya leo hata kesho!


Imeandikwa na ANTONY MWAKILIMA
Mawasiliano:   0756-351 462
                             0672-314 874
email; mwaijox@gmail.com


Comments

Popular posts from this blog

AVUMILIAYE MPAKA MWISHO NDIYE ATAKAYEOKOKA!

KIPIMO UNACHOPIMIA WENGINE NDICHO UTAKACHOPIMIWA

HASIRA HASARA