ANGALIA USIVYOVIONA

Angalia Usivyoviona!
Habari rafiki zangu? Ninayofuraha kuwashirikisha kuhusu kuangalia usivyoviona.

Unaweza kujiuliza utawezaje kuangalia usivyoviona. Kuangalia si lazima vionekane unapoamua kuangalia maana yake unaanza kuzingatia ni tofauti kidogo na kutazama ambapo ni lazima uone kile unachokitazama. Suala la kuangalia visivyoonekana ni suala ambalo humfanya mtu aanze kuona kwamba ili awe asivyoviona anahitaji kuwa tofauti.

Nini maana visivyoonekana?

Unajua maisha yako ya kesho ni Kitu ambacho hukioni, hizo ndoto ulizonazo za kutaka kuwa mtu mkubwa sana baadae ni Kitu usichokiona, hiyo mipango ya kumiliki jumba na magari ya kutembelea bado havionekani, unapoifikilia mbingu na uzima wa milele unapata picha ya vitu visivyoonekana,unaambiwa kuhusu imani ni lazima uanze kufikiria visivyoonekana, ukifuatilia vizuri vitu vingi usivyoviona ni vizuri mno, vinavutia, vinapendeza na kutia hamasa pia. Kama unatazamia kuwa mfanyabiashara mkubwa, msanii maarufu au mtu fulani mwenye hadhi kubwa, katika jambo lolote unalolifanya lazima ujifunze kuangalia usivyoviona.  Usipoangalia usivyoviona huwezi kuacha tabia ambazo zinakukwamisha usivione. Kuna mfumo wa maisha inabidi ubadilike kwa kifupi unatakiwa uvifanye visivyoonekana vionekane.
Sio kitu rahisi sana lakini ukishaanza kuacha kuangalia unavyoviona utaanza kujiweka tofauti kwa sababu vile usivyoviona ambavyo ndio vikubwa na vizuri vinakuhitaji uwepo katika mazingira ambayo yatavifanya vionekane.
Kuna maisha unaishi sasa kutokana na unavyoviona ni lazima mfumo wako ubadilike ili uone usivyoviona, iyo tabia ya uoga na kutothubutu inatokana na unavyoviona kwamba kuna MTU alifanya ikashindikana, hayo mazoea ya kutopenda kujifunza yanatokana na unavyoviona kwamba unaamini unavyojua inatosha, usiishi kwa mazoea unapoangalia visivyoonekana unaanza kujifunza zaidi kuhusu hivyo ili vionekane siku moja unaweka bidii zaidi ili kuhakikisha mpaka unaviona, unaacha uvivu, unaacha tabia ya kulaumu na kuacha kuongea badala ya kufanya hapo utaanza kupata matumaini ya kuona usivyoviona vikionekana.

Angalia visivyoonekana itakusaidia kutambua uishije, ili uweze kuzifikia ndoto, malengo, mipango na kesho uitakayo! Tuangalie tusivyoviona kwa sababu vinavyoonekana ni vya kitambo tu!

                      JITAMBUE!

Imeandikwa na Antony Mwakilima.
Mawasiliano:     0756 351 462
                             0672 314 874
email:     mwaijox@gmail.com      

       TAFAKARI BADILI MTAZAMO
                         ©2017

Comments

Popular posts from this blog

AVUMILIAYE MPAKA MWISHO NDIYE ATAKAYEOKOKA!

KIPIMO UNACHOPIMIA WENGINE NDICHO UTAKACHOPIMIWA

HASIRA HASARA