USIPUUZE HALI YOYOTE ISIYO YA KAWAIDA KIAFYA INAPO KUTOKEA
Ndio ni siku nyingine tena na wasaa mwingine MUNGU ametupatia nafasi ya kukutana katika blog yetu hii nzuri inayokuelimisha kwa habari za afya lakini tukilenga zaidi mafanikio.nikushukuru kwa kufanya uamuzi wa busara kwa kujipa muda huu wathamani sana kujifunza nasi kupitia makala hii nikukaribishe rasmi tuendelee na mada yetu. Ni kweli usipuuze inamaana sana kuutambua mwili wako unapokuwa na afya njema ili iwe rahisi kujua mambo yanapobadilika kiafya katika mwili wako afya inapoyumba .utajiuliza maswali mengi kwamba ni kwa nini nakuambia usipuuze,ni kwamba .... (A)kila hali isiyoyakawaida katika mwili wako inauwezo wa kuathiri utendaji wako wa kila siku.kutokana na udhaifu au unyonge wa mwili kuna mambo hautayafanya kwa viwango vinavyotakiwa japo utakuwa unajiona uko sawa kumbe sivyo.hali hiyo inaweza kukufanya ukawa mvivu kufanya kazi na kuathiri uzalishaji wako.Ndio ukiathiri uzalishaji unawaathiri wahitaji hivyo kama ni mkulima unamuathiri mfanyabiashara ambaye atahama kwako kwen...