USIPUUZE HALI YOYOTE ISIYO YA KAWAIDA KIAFYA INAPO KUTOKEA

Ndio ni siku nyingine tena na wasaa mwingine MUNGU ametupatia nafasi ya kukutana katika blog yetu hii nzuri inayokuelimisha kwa habari za afya lakini tukilenga zaidi mafanikio.nikushukuru kwa kufanya uamuzi wa busara kwa kujipa muda huu wathamani sana kujifunza nasi kupitia makala hii nikukaribishe rasmi tuendelee na mada yetu.


Ni kweli usipuuze inamaana sana kuutambua mwili wako unapokuwa na afya njema ili iwe rahisi kujua mambo yanapobadilika kiafya katika mwili wako afya inapoyumba .utajiuliza maswali mengi kwamba ni kwa nini nakuambia usipuuze,ni kwamba ....
(A)kila hali isiyoyakawaida katika mwili wako inauwezo wa kuathiri utendaji wako wa kila siku.kutokana na udhaifu au unyonge wa mwili kuna mambo hautayafanya kwa viwango vinavyotakiwa japo utakuwa unajiona uko sawa kumbe sivyo.hali hiyo inaweza kukufanya ukawa mvivu kufanya kazi na kuathiri uzalishaji wako.Ndio ukiathiri uzalishaji unawaathiri wahitaji hivyo kama ni mkulima unamuathiri mfanyabiashara ambaye atahama kwako kwenda kwingine pale hali yako ya kudhoofu itakapozidi kuwa mbaya zaidi kwa sababu licha ya kuwa dhaifu bado ukajilazimisha kufanya kazi nzito zilizoendelea kukudhohofisha ,unaposhituka udhaifu ni mkubwa na huwezi tena kuendelea na uzalishaji,lakini kumbe kama usingepuuza isingechukua muda kuirekebisha na kuendelea kuzalisha kama kawaida .
(B)Hali isiyoyakawaida  mwilini mwako inaweza kuwa ni dalili ya kutokea kwa tatizo kubwa la kiafya mfano ugonjwa wa kansa,hali hiyo ikipuuzwa hupelekea madhara ya kukomaa kwa ugonjwa kufikia hatua ya kutotibika ambapo yamkini kama usingepuuza ungeweza kutibiwa na  kupona kabisa.usisubiri ushindwe kufanya chochote ndipo ukaamua kujua chanzo cha tatizo.kuwa makini ni muhimu kulizingatia hili.
Kwani kufikia hatua hii inaweza kukugharimu maradufu kuliko ukaona bora ungewahi,mana hata mtaji wako/mshahara wako hautoshi kujitibia tatizo likapona kabisa,unapoteza mtaji na pia unapoteza thamani ya mwili wako...jihadhali usipuuze ni gharama kurejesha ubora wa mwanzo ,utapoteza pesa nyingi,muda mwingi,wateja wengi kiasi ambacho hata ukifanikiwa kupona utatakiwa kuanza upya...kutafuta mtaji na wateja...au kutafuta kazi kwa walioajiriwa maana mwenye kampuni hayuko tayari kuingia hasara kwa ajiri yako.
        usipuuze ni gharama.


Imeandikwa na  Antony Mwakilima
Mawasiliano:   0672 314 874 au
                             0756 351 462.
email:   mwaijox@gmail.com


          KWA PAMOJA TUNAWEZA

Comments

Popular posts from this blog

AVUMILIAYE MPAKA MWISHO NDIYE ATAKAYEOKOKA!

KIPIMO UNACHOPIMIA WENGINE NDICHO UTAKACHOPIMIWA

HASIRA HASARA