UKITAKA CHUMA KUWA SUMAKU
Habari yako mpendwa mfuatiliaji wa makala zetu za mafanikio,afya na tabia. Tunajua ili tufanikiwe kwenye yale tunayoyafanya tunahitaji watu ambao tutaendana nao kitabia, kiufanisi na kiuadilifu. Nakukaribisha tena siku ya leo tujifunze kutoka kwa sumaku. Kuna watu wanajiuliza nitamjuaje wa kufanana naye? Ninayeendana naye? Najua kuna mtu unamtafuta ufanye naye kitu mfano biashara, kuna mtu unamtafuta ujenge naye urafiki, uchumba n.k Yaani kuna sifa unatamani mtu Fulani awe nazo ndipo uweze kufanya naye jambo fulani kama mifano tajwa hapo juu. Nataka nikueleze, ukimkuta kichaa jaani hushangai, lakini mtu aliyetimamu ukimkuta huko bila shaka lazima ushangae. Ndio kuna mazingira ambayo huwezi kuwakuta nzi wako wengi kama mazingira machafu. Kuna watu unataka ushirikiane nao katika jambo kwenye maisha yako wakiwa na sifa fulani lakini unashindwa kuwajua. Iko wazi kwamba ndege wanaofanana ndio wanaoruka pamoja, swali ni je,utamjuaje binadamu unayefanana naye katika hilo unalotaka kulifan...