UKITAKA CHUMA KUWA SUMAKU

Habari yako mpendwa mfuatiliaji wa makala zetu za mafanikio,afya na tabia. Tunajua ili tufanikiwe kwenye yale tunayoyafanya tunahitaji watu ambao tutaendana nao kitabia, kiufanisi na kiuadilifu. Nakukaribisha tena siku ya leo tujifunze kutoka kwa sumaku.

Kuna watu wanajiuliza nitamjuaje wa kufanana naye? Ninayeendana naye?
Najua kuna mtu unamtafuta ufanye naye kitu mfano biashara, kuna mtu unamtafuta ujenge naye urafiki, uchumba n.k Yaani kuna sifa unatamani mtu Fulani awe nazo ndipo uweze kufanya naye jambo fulani kama mifano tajwa hapo juu. Nataka nikueleze, ukimkuta kichaa jaani hushangai, lakini mtu aliyetimamu ukimkuta huko bila shaka lazima ushangae. Ndio kuna mazingira ambayo huwezi kuwakuta nzi wako wengi kama mazingira machafu. Kuna watu unataka ushirikiane nao katika jambo kwenye maisha yako wakiwa na sifa fulani lakini unashindwa kuwajua.

Iko wazi kwamba ndege wanaofanana ndio wanaoruka pamoja, swali ni je,utamjuaje binadamu unayefanana naye katika hilo unalotaka kulifanya?

Tufikirie sifa za sumaku kidogo!
Sumaku inasifa au tabia yakuvuta vitu vyenye sifa ya kuvutwa na sumaku mfano chuma, nikeli, na kolbati. Huwezi kukuta sumaku inanasa mawe, wala shaba, wala mbao au kitu chochote ambacho hakina sifa ya kuvutwa na sumaku.
Sumaku kwa sumaku pia zinavutana tena mvutano wake ni mkubwa zaidi kuliko hata ule uliopo kati ya sumaku na chuma au nikeli au kolbati.

Tunajifunza nini kutokana na sifa za sumaku???
Tabia yako au sifa zako zinaouwezo mkubwa wa kukuamulia aina na sifa ya watu utakaoshirikiana nao. Wakati mwingine unaweza ukadhani hauna bahati kwa kuwa mara kwa mara umekuwa ukikutana na watu ambao unawaona sio sahihi kwako. Ukweli ni kwamba ili upate watu wenye tabia fulani lazima wewe uanze kuandaa mazingira yatakayomvuta mtu huyo kwa kuhakikisha unaanza kuwa na tabia hizo wewe kwanza. Sumaku inaweza kuvutwa kwa sumaku tu. Na sumaku haivuti kila kitu isipokuwa kile chenye sifa au tabia ya kuvutwa na sumaku pekee. Watu wenye sifa na tabia kama zako ndio pekee unaoweza kuwavuta kwako. Ukiona unataka mtu mwenye sifa usonazo wewe ujue unalo zoezi la kuwa na sifa zitakazomvutia kwako. Kwa hiyo sio rahisi nyuki kumfata mtu pasipo sababu lazima kuna harufu imemvutia sio rahisi kumkuta nyuki kwenye kila ua yapo maua ambayo ukimkosa nyuki humo unajiuliza imekuaje.

Jifunze kuwa sumaku uwavute kwako wenye tabia za kuvutwa nawe au uvutwe na wenye tabia kama yako.
Tabia zikifanana ni rahisi kuendana kuvutana na kuelewana. Rekebisha hapo kwanza uone kama hawatakuja unaowataka. Na hii ndio njia pekee na rahisi ya kuwapata wenye tabia unazotaka lazima uanze wewe. Yangeyange mara nyingi huruka kwa makundi kama ujuavyo wale ndege ni weupe pee, kwa hiyo wakiwa kwenye kundi ni rahisi kumjua ndege aliyezamia lakini kumkuta ni nadra sana.

Tambua mwenye sifa unazozitaka anamtafuta mwenye sifa kama hizo ili ashirikiane naye kwa hiyo sumaku hunasa sumaku au chuma, wakati huo sumaku kama zinaweza kunasana kumbe nazo zina sifa ya chuma ndani yake.Pia ni rahisi sumaku kunasa sumaku kuliko Kitu kingine hata chuma chenyewe. Utaendelea kulaumu hupati watu sahihi kumbe UKITAKA CHUMA SHARTI UWE SUMAKU NI KUAMBUKIZANA na KUNASANA tu.

Urahisi uliopo ni kwamba maeneo unayoweza kupata chuma ni tofauti na maeneo unayoweza kupata kolbati  na pia ni tofauti na ilipo nikeli. Kwa hiyo sio rahisi kuvivuta vyote kwa pamoja.
Kikubwa uwe nikeli au chuma au kolbati ili uweze kukivuta kimoja wapo.

Imeandikwa na Antony Mwakilima.
Mawasiliano:     0756 351 462
Whatsapp          0783 153 224
email:     mwaijox@gmail.com      

       TAFAKARI BADILI MTAZAMO
                         ©2017

Comments

Post a Comment

Popular posts from this blog

AVUMILIAYE MPAKA MWISHO NDIYE ATAKAYEOKOKA!

KIPIMO UNACHOPIMIA WENGINE NDICHO UTAKACHOPIMIWA

USIMDHARAU MTU YEYOTE