Posts

Showing posts from 2021

CHANGAMOTO ZIPO

Habari ya wakati huu rafiki yangu mpenzi msomaji wetu wa makala katika mtandao huu? Natamani kukushirikisha juu ya mambo haya kuhusu changamoto kwenye maisha yako. Ugumu wa changamoto uliyonayo unaendelea kuongezeka kutokana na kutokufahamu mambo yafuatayo. KUKUBALI CHANGAMOTO Awali ya yote ni lazima ujifunze kukubali kuwa hakuna jambo kubwa au dogo utakalolifanya litakosa changamoto . Kwa kifupi huwezi kuzikimbia changamoto kwa namna yoyote ile badala yake jifunze kukubali kuwa changamoto zipo na ni lazima uzikabili na Kuzishinda. Kwa nini kukubali changamoto ? Nakushauri ukubali kwanza changamoto zipo ili uweze kujiandaa kisaikolojia ijapo ikukute u tayari kuipokea na kukabiliana nayo. Mfano wa Donald Trump kama hasingekubali changamoto yamkini hasingeshinda uraisi huko Marekani! JIFUNZIE CHANGAMOTO Pili ni lazima ujifunze kuwa unapopitia magumu au tabu Fulani kwenye maisha ni fursa ya wewe kujifunza jambo jipya. Badala ya kuutazama ugumu ulionao na kukata tamaa, jiulize