CHANGAMOTO ZIPO

Habari ya wakati huu rafiki yangu mpenzi msomaji wetu wa makala katika mtandao huu? Natamani kukushirikisha juu ya mambo haya kuhusu changamoto kwenye maisha yako.

Ugumu wa changamoto uliyonayo unaendelea kuongezeka kutokana na kutokufahamu mambo yafuatayo.

KUKUBALI CHANGAMOTO
Awali ya yote ni lazima ujifunze kukubali kuwa hakuna jambo kubwa au dogo utakalolifanya litakosa changamoto. Kwa kifupi huwezi kuzikimbia changamoto kwa namna yoyote ile badala yake jifunze kukubali kuwa changamoto zipo na ni lazima uzikabili na Kuzishinda. Kwa nini kukubali changamoto? Nakushauri ukubali kwanza changamoto zipo ili uweze kujiandaa kisaikolojia ijapo ikukute u tayari kuipokea na kukabiliana nayo. Mfano wa Donald Trump kama hasingekubali changamoto yamkini hasingeshinda uraisi huko Marekani!

JIFUNZIE CHANGAMOTO
Pili ni lazima ujifunze kuwa unapopitia magumu au tabu Fulani kwenye maisha ni fursa ya wewe kujifunza jambo jipya. Badala ya kuutazama ugumu ulionao na kukata tamaa, jiulize unakosea kitu gani, na kwa nini, na ufanye nini? Kisha jifunze. Ni kweli kabisa utaweza kujifunza mambo mengi sana kupitia changamoto yako mfano wa mambo ya kujifunza kutegemeana na changamoto husika ni kuishi vizuri na watu,kuacha ubinafsi,kuwajua wanafiki, kuchagua marafiki wa kushirikiana nao, na jinsi ya kurekebisha chanzo cha tatizo na kuepuka lisitokee tena.

UTAMBUE UWEZO WAKO
Tatu ni muhimu sana kujua kuwa changamoto uliyonayo si zaidi ya uwezo ulionao kupambana nayo na kuishinda.
Yaani hakuna! hakuna! hakuna! jambo kubwa kwenye maisha yako kama uwezo wako. Ukitambua uwezo wako hutakaa kuogopa changamoto yoyote ile kwa sababu unajua hakuna changamoto itakayokutisha wala kukukatisha tamaa kwa vile unajua changamoto zote katika maisha yako yapo chini au ndani ya uwezo wako. Kwa kujua hayo hutaiona changamoto kama changamoto Bali kama kipimo cha uwezo ulionao katika kufikiri, kuvumilia, na kuamua.

CHANGAMOTO HAZIWEZI KUFANANA
Ni dhahiri kuwa katika maisha tupo watu wenye weredi ,mtazamo, mbinu,uwezo utalaamu na uelewa/maarifa tofauti na mbalimbali. Hivyo basi utofauti huu ndio unaozitofautisha changamoto kwenye maisha yetu. Yamkini changamoto ulizonazo na mwingine pia anazo lakini zikatofautiana uzito kutokana na ule utofauti wa ndani kati ya mtu mmoja na mwingine kiuwezo. Unapoiona changamoto usiogope,usiikwepe kwa sababu hakuna mwingine atakayeishinda changamoto hiyo ila ni wewe na hakuna mwingine atakayekusaidia kuipitia changamoto yako. Ndio maana Yesu alipowahusisha wanafunzi wake kuomba pamoja nae haikuwa rahisi kwa sababu ile changamoto haikuwa ya wote Bali peke yake naye ndiye aliyekuwa na uwezo kuishinda.

CHANGAMOTO NI FURSA
Uwapo katika jamii ni muhimu kujifunza kuiangalia changamoto kama fursa badala ya kikwazo au kizuizi cha wewe kufika mahali Fulani unataka ufike kwenye maisha yako. Ukiitazama changamoto kama fursa inakusaidia kuwa na maono makubwa hususan kuwa na shauku ya kuisaidia jamii yako kuondokana na changamoto hizo. Usiione kama tatizo,jipe muda ichunguze ifanye fursa isaidie jamii yako nayo itakulipa kwa kuiondoa changamoto miongoni mwao.

CHANGAMOTO NI UJUMBE.
Inawezekana ukajiuliza ni kwa namna gani uichukulie changamoto kama ujumbe kwako,jibu ni rahisi tu,changamoto uliyonayo inaweza kukupa ujumbe Fulani  ukianza kudadisi kwa nini IPO,mfano kwa watumishi wa MUNGU kuna changamoto wanazipitia sababu kuna mahali walikosea au wamemkosea MUNGU pia wewe na Mimi tunapomkosea MUNGU au kuacha kumtegemea kunasababisha tupitie changamoto Fulani hivyo basi changamoto hizo zinaweza kuwa ujumbe kwetu kwamba tumemkosea MUNGU,hasara kwenye biashara ni changamoto inatupa ujumbe kwamba kuna mahali tunakosea labda tumechanganya familia,urafiki na biashara,hatutunzi rekodi,hatujali wateja au hatutoi hiduma ya kiwango stahiki,tunashirikiana na matapeli au (partners)wasiofaa n.k pia katika maisha ya kawaida zipo jumbe mbalimbali ambazo tunaweza kuzipata kutokana na changamoto tunazozipitia mfano uache umimi au ubinafsi,usiwe na dharau ,ushirikiane na jamii n.k
Hizo ni baadhi tu ya jumbe zitokanazo na changamoto tunazozipitia na hivyo ndivyo utakavyoweza kuzitambua.
Mara utambuapo jumbe zozote kutokana na changamoto yako ,chukua tahadhari, jirekebishe na utubu.

JINSI YA KUZIKABILI CHANGAMOTO
Naam,mtazamo chanya pekee ndio jibu la utatuzi wa tatizo au changamoto yoyote unayokutana nayo kwenye maisha yako.
Jiulize huwa unaichukuliaje changamoto?unafanyaje kukabiliana nayo?

Hivyo ndivyo Mimi ninavyoiona changamoto kwangu,wewe unaionaje?
Ni hamu yangu sote tuione changamoto kwa namna hiyo na tuwe na mtazamo chanya juu ya mambo mbalimbali tunayoyapitia, ukiwa chanya unajiweka kwenye mazingira ya kuishinda changamoto hata kabla haijatokea.

Karibu sana!

Imeandikwa na Antony Mwakilima.
Mawasiliano:     0756 351 462
                             0672 314 874
email:     mwaijox@gmail.com

         KWA PAMOJA TUNAWEZA

Comments

Popular posts from this blog

AVUMILIAYE MPAKA MWISHO NDIYE ATAKAYEOKOKA!

KIPIMO UNACHOPIMIA WENGINE NDICHO UTAKACHOPIMIWA

HASIRA HASARA