Posts

Showing posts from January, 2017

USIANGALIE ULIONAO ANGALIA WATAKAOKUJA

Habari ya siku ya leo mpendwa msomaji wa makala mbalimbali katika blog yetu?ni matumaini yangu kuwa uko vizuri na unaendelea kupambana kuhakikisha unakuwa na maisha unayoyataka lakini kwa ajili ya wengine yaani watu wa kundi lako. Karibu tena tuendelee kuongeza thamani kwenye maisha yetu. Haijalishi ulikuwa na kundi LA watu au marafiki kiasi gani kwenye maisha yako Jana. Maamuzi yako yatakayoibadilisha kwanza Leo na kuleta kesho mpya yanayo matokeo mawili. (1) Yanaweza kupelekea kuongezeka kwa marafiki wapya au idadi ya watu wa kundi lako . Hili likitokea wengi hatuna mashaka wala hatuogopi na tunaona ni kawaida na maisha yanaendelea. Yamkini iko hivi kwa sababu bado unaeleweka yaani hujabadilika umeendelea kuwa yuleyule kila siku hata ukiamua kubadilika unabadilika kidogo sana bila kuathiri maisha ya hilo kundi ulilonalo na pia inawezekana ukaona kawaida kwa sababu kila siku marafiki huongezeka, inabidi utambue sio kawaida ukiona kundi lako linaongezeka ujue unahitaji nguvu zaidi

UNAVYOTOA SI SAWA NA WANAVYOPOKEA

Ninayofuraha kukualika tena rafiki mpendwa mfuatiliaji wa makala zetu,ni imani yangu kuwa wewe ni mzima wa afya kabisa na unaendelea vizuri katika yote unayojishughurisha nayo kuhahakikisha unafikia mafanikio yale uyatakayo. Ni siku nzuri tena ninayotaka tushirikishane juu ya unavyotoa kwa wengine na namna ambavyo wanavipokea na ukubwa ambao wanavichukulia vile unavyovitoa. Ni mara nyingi sana watu wengi wamekuwa wanashindwa kutoa kwa sababu wanadhani kwamba kila anayepewa anahitaji kikubwa ili aitambue thamani ya mtoaji. Nimekuwa shahidi wa jambo hili ndio maana nimeamua nikushirikishe ili tupate ufahamu huu wa ajabu ,mimi nimejifunza kwamba inapofikia hatua ya kumfanyia mtu kitu watu wengi tumekuwa na kasumba ya kujithaminisha kwa kuangalia kazi au shughuri unazofanya na jinsi ambavyo mtu huyo unayetaka kutoa kwake mnaheshimiana kiasi gani? au atakuchukuliaje ukitoa kwake hicho unachotaka kutoa? Yawezekana umefikia hatua hii kwa sababu unadhani unachotaka kutoa ni kidogo sana na k

USIACHE KUWA MTOTO KWA WAZAZI WAKO

Ahsante sana mpenzi msomaji kwa kuendelea kujifunza pamoja nasi yale yanayotuwezesha kuwa na maisha bora yenye furaha kila iitwapo leo, sina shaka u mzima wa afya kabisa. Naomba nikukaribishe kwenye mada ya leo ambayo tunakwenda kujifunza habari ya kuendelea kuwa mtoto kwa wazazi wako , kusema hivi haina maana ya kuendelea kudeka kwa wazazi wako,kuendelea kuwategemea kwa kila unachokihitaji au kuendelea kuwapa mzigo wa kukulea ungali mtu mzima ambaye unayomajukumu na unauwezo wa kujitegemea kimaisha bali namaanisha kwamba kuna hatua za kimaisha watu wakifikia husahau kabisa kuwa wao ni watoto kwa wazazi wao na kwamba haijalishi wana nafasi gani kwenye jamii yao wataendelea kuwa watoto kwa wazazi wao. Kuna mambo mengi yamepelekea watu wakasahau kuwa wanapofika kwa wazazi wao wanaendelea kuwa watoto na pia inawapasa waendelee kuwaheshimu na kuwanyenyekea hata kuwa msaada kwao kwa kubeba jukumu la malezi pale wanapokuwa hawawezi tena yaani wamezeeka au hawana nguvu tena za kuwasaidia