USIACHE KUWA MTOTO KWA WAZAZI WAKO

Ahsante sana mpenzi msomaji kwa kuendelea kujifunza pamoja nasi yale yanayotuwezesha kuwa na maisha bora yenye furaha kila iitwapo leo, sina shaka u mzima wa afya kabisa.

Naomba nikukaribishe kwenye mada ya leo ambayo tunakwenda kujifunza habari ya kuendelea kuwa mtoto kwa wazazi wako, kusema hivi haina maana ya kuendelea kudeka kwa wazazi wako,kuendelea kuwategemea kwa kila unachokihitaji au kuendelea kuwapa mzigo wa kukulea ungali mtu mzima ambaye unayomajukumu na unauwezo wa kujitegemea kimaisha bali namaanisha kwamba kuna hatua za kimaisha watu wakifikia husahau kabisa kuwa wao ni watoto kwa wazazi wao na kwamba haijalishi wana nafasi gani kwenye jamii yao wataendelea kuwa watoto kwa wazazi wao.

Kuna mambo mengi yamepelekea watu wakasahau kuwa wanapofika kwa wazazi wao wanaendelea kuwa watoto na pia inawapasa waendelee kuwaheshimu na kuwanyenyekea hata kuwa msaada kwao kwa kubeba jukumu la malezi pale wanapokuwa hawawezi tena yaani wamezeeka au hawana nguvu tena za kuwasaidia kupambana na maisha yao. Mfano wa mambo hayo ni kama ifuatavyo;

VYEO                                                        
Ndio ni kweli watu wengi wamekuwa ni wenye nidhamu hasa pale wanapokuwa katika mazingira ya maisha ya kawaida ,yaani wakiwa hawana kazi au cheo chochote au wakiwa bado wanaishi na wazazi wao. Hapo wengi wetu tunakuwa ni wenye kuwapenda,kuwaheshimu na kuwathamini sana wazazi wetu lakini tunapoingia kwenye majukumu ya kiofisi na vyeo tunaanza kubadilika.Mfano ulikuwa unapenda sana kuwa nao karibu na ukawa unatekeleza hilo unaanza kukaa muda mrefu sana pasipokuwatembelea wazazi wako ukisingizia majukumu ni mengi,ni kweli majukumu ni mengi lakini je yanapaswa kubadili mfumo wako wa maisha ? Ni kweli una cheo na wengi wanakuheshimu,je ndicho kinachoishusha heshima yako kwa wazazi wako? La!si lazima cheo chako kikubadlishie mfumo wa maisha na pia kikufanye uache kuwathamini na kuwaheshimu uliokuwa unawatendea hayo kabla, cheo ni hatua kama kinavyokuja ndivyo kinavyoweza kuondoka lakini wazazi wako wanabaki kuwa wazazi wako tu. Usisubiri kwanza uwe na shida upatwe na magumu au ushindwe ndipo uwakumbuke.Waheshimu sana wazazi wako kwa cheo chako hata kama wanaishi maisha magumu au ya kimaskini ni wazazi tu na wanahitaji uwekaribu nao.

UMAARUFU                                                   
Kitu kingine ambacho kimewapoteza watu wengi na kuwafanya waache kuwa watoto kwa wazazi wao ni umaarufu. Wengi wanapopata umaarufu au wanapojulikana kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo usanii au utajiri wanaacha kuwa watoto kwa wazazi wao. Kuna mambo mengi ambayo tumekuwa tunayafanya wakati hatujapata maisha mazuri zaidi kama tulionayo sasa na mambo haya yamekuwa ni msaada mkubwa kwa wazazi wetu kiasi ambacho wameendelea kutuona kuwa tu watoto wao mfano tulipowatembelea hatukusita kufanya shughuri mbili tatu za kuwasaidia wazazi wetu na pia tulikuwa na muda mwingi wa kuzungumza nao na kuwashirikisha kuhusu maisha yetu lakini kinachosikitisha ni pale tunapobadilika baada ya kuifikia hatua nzuri ya maisha ambapo ingefaa sana hata kuchukua jukumu la kuwalea badala yake tunadumazwa na umaarufu tunawasahau na kuwaacha pasipo msaada wowote na bado tunaendelea kutamani kuishi maisha marefu yenye Baraka tele,hakika tunajidaanganya kabisa.

ULIMBUKENI
Kuna wengine kutokana na ulimbukeni wa mjini watoka makwao huko vijijini wamezamia mijini na huko wakapata sehemu za kujishikiza wakasahau walikotoka na hali ambazo wameziacha kwa wazazi wao. Pindi tunapokuwa vijijini mwetu tunaonekana ni watu wenye kujali wazazi wetu hata tunapofanya vibarua tukipata chochote tunawakumbuka wazazi wetu lakini baada ya kwenda maeneo Fulani tofauti kidogo na nyumbani kimaisha tunaacha yale tuliyokuwa tukiyafanya kwa wazazi wetu tunafuata maisha ya watu wengine na bado tunaamini kesho tutatoka na kufanikiwa wakati huo hatuwaheshimu wazazi wala kuwathamini tena.Katika hatua hii watu huacha hata kule kujitoa kwa ajili ya wazazi wao na kuna shughuri ambazo awali walizifanya kwa wazazi wao lakini sasa hawako tayari tena kuzifanya na wanaona hawana hadhi hiyo hawakumbuki tena kuwa wao ni watoto kwa wazazi siku zote.

ELIMU
Kuna wengi wakielimika

Kwa nini tubaki watoto kwa wazazi wetu?                                                                 Ni kwa sababu sisi sote tunahitaji mambo makubwa mawili ambayo hatuwezi kuyapata popote isipokuwa tumeheshimu wazazi wetu,

MAFANIKIO,KHERI au BARAKA
Ndio tunapowaheshimu wazazi wetu tunaouhakika wa kupata maisha ya kheri na Baraka lakini pia yenye mafanikio na furaha.Watu wengi wameliona hili kuwa ni jambo la kawaida wamelinyima uzito lakini kwa kiasi kikubwa sana limechangia maisha yetu kuwa ya hovyo na kutokufanikiwa.Si kitu kingine ila ile heshima inapokosekana tunapata laana ya maisha tunazipoteza zile Baraka ambazo hutokana na sisi kuendelea kuwa watoto kwa wazazi wetu. Wakati mwingine tunakazi nzuri au maisha mazuri lakini wazazi wetu wanaishi maisha magumu yaliyotawaliwa na umaskini wala hatuchukulii kama ni jukumu letu kuwajali na kuwalewa wazazi wetu pale tunapoona hawawezi si kwa maana ya kurudisha fadhila lakini ni kwa maana ya kutimiza majukumu yako kama mtoto kwa mzazi.

KUISHI SIKU NYINGI au MAISHA MAREFU
Hakika sisi sote tunapenda kuishi maisha marefu hasa tunapokuwa tumefanikiwa. Kuishi vizuri na kwa heshima na wazazi wako unajiwekea uhakika wa kuishi maisha yaliyojaa siku nyingi zenye mafanikio au Baraka nyingi. Inasikitisha wengi wanapofanikiwa hawadumu sana ndani ya mafanikio yao na ukiangalia yamkini hawakuwaheshimu wazazi wao na kwa kulithibitisha hili wapo ambao wametajirika kutokana na masharti na moja ya masharti hayo ni kuja kuwatoa wazazi wao sadaka, bila shaka jambo hili si geni kwako. Watu wengi wa jinsi hii hawadumu yaani wasiokubali kuendelea kuwa watoto kwa wazazi wao.
Ukitaka maisha marefu yenye Baraka Duniani,waheshimu wazazi wako na uwe kwao mtoto siku zote. Vyeo, umaarufu, ulimbukeni au nafasi yoyote uliyonayo kwenye jamii isikufanye ukaacha kuwaheshimu wazazi wako na kuwa mtoto kwao kwa kutimiza majukumu yako kwa wazazi wako.

Imeandikwa na Antony Mwakilima
Mawasiliano:    0756-351 462  
                           0672-314874                         
email:mwaijox@gmail.com
                                                 
          KWA PAMOJA TUNAWEZA
                          ©2016
                         

Comments

Popular posts from this blog

AVUMILIAYE MPAKA MWISHO NDIYE ATAKAYEOKOKA!

KIPIMO UNACHOPIMIA WENGINE NDICHO UTAKACHOPIMIWA

HASIRA HASARA