Posts

Showing posts from October, 2016

THAMANI UNAYOTOA SI SAWA NA WANAYOIPOKEA

Image
Ninayofuraha kukualika tena rafiki mpendwa mfuatiliaji wa makala zetu,ni imani yangu kuwa wewe ni mzima wa afya kabisa na unaendelea vizuri katika yote unayojishughurisha nayo kuhahakikisha unafikia mafanikio yale uyatakayo. Ni siku nzuri tena ninayotaka tushirikishane juu ya unavyotoa kwa wengine na namna ambavyo wanavipokea na ukubwa ambao wanavichukulia vile unavyovitoa. Ni mara nyingi sana watu wengi wamekuwa wanashindwa kutoa kwa sababu wanadhani kwamba kila anayepewa anahitaji kikubwa ili aitambue thamani ya mtoaji. Nimekuwa shahidi wa jambo hili ndio maana nimeamua nikushirikishe ili tupate ufahamu huu wa ajabu ,mimi nimejifunza kwamba inapofikia hatua ya kumfanyia mtu kitu watu wengi tumekuwa na kasumba ya kujithaminisha kwa kuangalia kazi au shughuri unazofanya na jinsi ambavyo mtu huyo unayetaka kutoa kwake mnaheshimiana kiasi gani? au atakuchukuliaje ukitoa kwake hicho unachotaka kutoa? Yawezekana umefikia hatua hii kwa sababu unadhani unachotaka kutoa ni kidogo sana na

FANYA UNACHOKIPENDA

Habari ya leo tena mpendwa msomaji na rafiki yangu ?ni matumaini yangu kuwa uko na afya njema kabisa inayoimarika kila siku kwa ajili ya kukuwezesha kuweka bidii zaidi hata kufikia mafanikio uyatakayo. Ni vema sana kuupa mwili wako kile unataka kwa ajili ya kuwa na afya njema ,nguvu na kukupa ujasiri wa kupambana mpaka umeona mafanikio au umepata kile unachotaka. Fanya unachopenda mwenyewe. Nasisitiza tena fanya unachokipenda wewe mwenyewe.Hapa nazungumzia habari ya kufanya chochote halali chenye matokeo chanya kwenye maisha yako na yanayokuzunguka,kuna mambo mengi mazuri unatamani kuyafanya kutoka moyoni mwako lakini pengine umekutana na wanaokupinga usifanye au wanaokuzuia kufanya hicho kisichoharamu unachopenda kufanya. kwa nini ufanye unachokipenda? Kufanya unachokipenda itakufanya 1/uweke bidii kubwa tofauti na yule anayefanya kitu asichokipenda au anayeshinikizwa kufanya jambo asilolipenda. Ndio wengi wameshindwa kutimiza ndoto zao au maono yao ya kimaisha kutokana na kufan

ATHARI HASI KUTOKANA NA WATU WAKO WA KARIBU

Image
Natumaini kuwa hujambo na unaendelea vizuri na mapambano ya maisha kuhakikisha unapata unachotaka. Nashukuru Mungu ni siku nyingine njema ambayo tunaendelea kujifunza juu ya mambo ambayo hutusaidia kufikia vilele vya mafanikio tunayoyataka.                        Ndio kuna athari nyingi hasi ambazo zimetokana na ndugu zetu,rafiki zetu,wapenzi wetu ,wazazi wetu pia ambazo zimechangia kuwa na maisha tuliyonayo sasa aidha kwa ushawishi wao kwako juu ya kile wanachokiamini au kwa shinikizo kutoka kwao ufanye kipendacho roho zao. Wapo ambao wamekushurutisha au kukulazimisha na kukushinikiza kufanya jambo ambalo moyo wako haukuwa tayari wala wewe binafsi hukulipenda lakini kwa heshima yao ukafanya ili waridhike bila kujua kwamba kufanya kitu usichopenda ambapo unakuwa hauko tayari, hauna amani na hufurahii kufanya kunapunguza ufanisi, ubunifu na ueledi wako kwa jambo ulipendalo. Kuna watu wameolewa kwa kulazimisha aidha kutokana na umasikini au tamaa za wazazi wao,wengine wameachana na we

ACHA KUTAMANI KUWA KAMA MWINGINE.

Habari ya wasaa huu rafiki zangu naimani nyote hamjambo na mnaendelea kuyafanyia kazi tunayojifunza kila wakati,nataka tujifunze kuhusu saikolojia ya kutammani kuwa kama mtu fulani au mtu mwingine,saikolojia hii ni kwamba hutafanya cha kwako ila cha yule unaetamani kuwa kama yeye. Ndio ni muhimu sana kulitambua hili usitamani kuwa kama mimi na mimi nisitamani kuwa kama wewe kwa sababu ifuatayo ,kama mimi nikitamani kuwa kama wewe ,je ni nani atakayefanya kile Mungu amekusudia kifanyike kupitia mimi?pia kama wewe ukitamani kuwa kama mimi nani basi atakayefanya kile ambacho Mungu ametaka kifanyike duniani kupitia wewe?.Hii ndio sababu muhimu ya kukwambia usitake kuwa kama yeyote yule kwa kuwa hakuna kama wewe mwingine yaani wewe au mimi ni watofauti sana ukilinganisha na mwingine,na huo utoafauti wetu ndio thamani yetu.Kile kitu kinachokutofautisha na mimi ndio kitu kinachoutambulisha ubora wako ,thamani yako, uwezo wako na yamkini upekee ulionao. Kila mtu duniani amepewa kitu cha kufa