Posts

Showing posts from November, 2016

USIMDHARAU MTU YEYOTE

Habari yako mpenzi msomaji wetu?Bila shaka u mzima wa afya.Ni wakati mwingine tena siku nyingine tukiwa na hamasa nyingine nakukaribisha tuungane pamoja kujifunza juu ya usimdharau MTU yeyote! USIMDHARAU MTU Ndio natumaini kila mmoja wetu kama binadamu yawezekana kabisa kuna mazingira umekutana nayo kwenye maisha ukawadharau wengine au kuna Hadhi umepata ikakupelekea uone wewe pekee ndio unamaana na umuhimu.Nataka nikuambie usimdharau mtu awayeyote kwa sababu, Bado hujajua kila Kitu Yawezekana kwa hilo ulifanyalo wapo wenye maarifa zaidi ukiwadharau hutayapata.usijione kwamba huwezi tena kuhitaji maarifa yoyote kutoka kwa wengine, ni muhimu sana kujua hili ikiwa unataka kufanikiwa ni lazima uwe mchezaji mzuri wa timu yako ,maarifa yetu yanatofautiana na uwezo wa kufanya mambo vilevile kwa hiyo badala ya kudharauliana,golikipa anapaswa asimdharau mfungaji wake ama beki ili waweze kushirikiana vizuri hebu tushikane mikono kama timu tucheze pamoja ndivyo wengine wanavyofunga mago...

HASIRA HASARA

Image
Habari za leo rafiki yangu!bila shaka uko vizuri na unapiga hatua kila unaporuhusu ubongo wako upokee vitu vipya na kukuongezea thamani katika maisha yako. Leo ni siku nyingine tena tunayofuraha kuungana pamoja kujifunza kuhusu hasira hasara ,hebu jiulize ni mara ngapi umeruhusu hasira iamue juu ya hatima ya maisha yako licha ya kuijua methali hii? unadhani maamuzi uliyochukua ukiwa na hasira yamekuwa chanya kwenye maisha yako? kama hasira imekupa athari hasi za maamuzi uliyochukua ukiwa umeudhiwa ,umechukua hatua gani hata sasa? Naomba upate muda utafakari kiasi ambacho maisha yako yameathiriwa kutokana na maamuzi uliyofanya ukiwa na hasira, hebu mtazame Kaini alichofanya baada ya kutawaliwa na hasira alimuua nduguye Abeli, na baada ya hapo akaingia kwenye laana ambayo hakika ilisababisha maisha yake yasiende vizuri. Yawezekana kabisa alijua kwamba akiua ndugu yake mambo yake yatakuwa mazuri na pengine atakubalika badala yake kampoteza ndugu na laana juu. Je,ni mara ngapi umesikia ...

AVUMILIAYE MPAKA MWISHO NDIYE ATAKAYEOKOKA!

Habari ya uzima mpenzi msomaji wa makala zetu,tunayofuraha kuzidi kuendelea kujifunza pamoja nawe.Siku ya leo ni siku ya pekee kabisa ambayo tunakwenda kuzungumzia habari ya kuvumilia mpaka mwisho. Kuvumilia ni kule kukabiliana na changamoto zozote unazokutana nazo pasi na kukata tamaa,kurudi nyumba au kukubali kushindwa. Anayevumilia ni yule asiyekuwa tayari kushindwa licha ya ugumu anaoupitia. Kuvumilia kuna ukomo tofauti tofauti kulingana na mtu binafsi na ugumu husika anaoupitia. Kwa uzito uleule wa kazi fulani au changamoto fulani,wapo watu wa makundi yafuatayo kuhusiana na viwango vya uvumilivu wao. WANAOVUMILIA MUDA MFUPI TU. Kuna wengine huweza kuvumilia changamoto kwa muda mfupi tu na kukata tamaa au kuchoka kabisa na asiwe tayari kuendelea tena. Hawa wengi wao wanakuwa bado hawajayakaribia mafanikio kabisa yaani wanapothubutu tu kufanya jambo la kuwapeleka kwenye mafanikio, wakikutana na changamoto hukimbia kana kwamba wanapokimbilia hakuna changamoto. Hawa wanadhani ...

SIKU YA FURAHA NI LEO

Ninayofuraha siku nyingine tena kushirikiana ujumbe huu pamoja nawe mpenzi msomaji wa makala katika blog yetu,sina shaka unaafya njema na unaendelea kuweka bidii kwa ajili ya kuifikia safari ya mafanikio tuyatakayo! Ndio siku ya furaha ni leo! Tunapaswa kuiishi leo kana kwamba ni siku ya mwisho,tukiishi kwa furaha! Lazima usahau kuhusu jana ndipo unaweza kuishi leo vizuri na kwa furaha kwa sababu, Jana imekuwa ni siku ya kuumiza kwako,umeumizwa kwa mambo mengi mfano mahusiano, dhuluma, magonjwa, kuonewa, kushindwa na kukatishwa tamaa, kukataliwa n.k Jana imekuwa ni siku ya huzuni sana kwako,umehuzunishwa na misiba ya watu waliokuwa msaada wako wa karibu, unafiki wa marafiki na wale uliowaamini, ugumu wa maisha, utawala wa rushwa n.k Jana imekuwa ni siku ilijaza moyo wako uchungu kutokana na mateso ya mama wa kambo, ndugu wenye roho mbaya, kuibiwa na kunyang'anywa haki, kunyanyasika kutokana na hali ya umaskini,kupanda kwa gharama za maisha n.k Kuna wakati kutokana na jana iki...