Posts

Showing posts from February, 2017

KAZA MKANDA VIZURI

Habari za Leo mpenzi na mfuatiliaji wa makala za blog yetu! Ni matumaini yangu u bukheri wa afya njema. Ningependa nikukaribishe kwa mara nyingine tujifunze zaidi, kwa ajili ya kuendelea kupiga hatua mbele zaidi. Mungu awe pamoja nawe karibu! Kaza mkanda vizuri Najua kuna wakati umekuwa ukisafiri kondakta akakwambia funga mkanda. Ni kweli ni vizuri kufunga mkanda uwapo safarini hata kama hukai siti za nyuma ya gari lakini kufunga mkanda kunasaidia kupunguza mitikisiko na mishituko inayoweza kujitokeza aidha gari ikipitishwa kwenye bamzi unakuwa salama ,na Mimi nasisitiza usifunge tu hakikisha unakaza kabisa mkanda bila kujali uko siti gani . Si kwa manufaa yangu wala kondakta Ila ni kwa faida yako mwenyewe. Ninahakika umezoea kuona mikanda ikifungwa hasa kwenye suruali zenye viuno vikubwa kuliko cha mvaaji. Leo nataka nikwambie hata kama suruali yako unahisi haihitaji mkanda kwa kuwa imekukaa vizuri nakuambiaje funga mkanda na ukaze vizuri, hakuna anayejua badae kutatokea nini hiv

USIOGOPE

Habari za wakati huu mpenzi msomaji na mfuatiliaji wa makala zetu. Ninayo imani kuwa uko vizuri kiafya na unaendelea kupambana. Karibu tushirikishane jambo hili. Kama kipo Kitu MUNGU anathamini kwenye maisha ya kwako basi ni ule mpango yuko nao juu yako. Kuna watu ambao umewaamini sana,ni watu wa karibu,mke au mume, wazazi,mpenzi, ndugu ,marafiki zetu tumewashirikisha kuhusu maisha yetu na mipango tuliyonayo na yamkini tukadhani tungepata kusaidika na badala yake, tumepata matokeo kinyume na taraja letu. Natamani nikutie moyo kwamba kama suala la mipango ya MUNGU kwetu lingekuwa la kawaida kwake basi isingekuwa rahisi, Yusufu kuweza kuwa waziri mkuu na hatimaye ndugu zake kuwa chini yake kama MUNGU alivyokuwa amemuonesha kwenye maono kupitia njozi zake. Kwa sababu alipowashirikisha ndugu zake walikuwa tayari hata kumuua ili kile MUNGU amekusudia kwa Yusufu kisitokee. Ayubu pia asingeweza kushinda jaribu alilopitia hususan ni pale ambapo mkewe anamshawishi amkufuru MUNGU ili afe, n

ACHA KUTAMANI KUWA KAMA MWINGINE.

Habari ya wasaa huu rafiki zangu naimani nyote hamjambo na mnaendelea kuyafanyia kazi tunayojifunza kila wakati,nataka tujifunze kuhusu saikolojia ya kutamani kuwa kama mtu fulani au mtu mwingine,saikolojia hii ni kwamba hutafanya cha kwako ila cha yule unaetamani kuwa kama yeye. Ndio ni muhimu sana kulitambua hili usitamani kuwa kama mimi na mimi nisitamani kuwa kama wewe kwa sababu ifuatayo ,kama mimi nikitamani kuwa kama wewe ,je ni nani atakayefanya kile Mungu amekusudia kifanyike kupitia mimi?pia kama wewe ukitamani kuwa kama mimi nani basi atakayefanya kile ambacho Mungu ametaka kifanyike duniani kupitia wewe?.Hii ndio sababu muhimu ya kukwambia usitake kuwa kama yeyote yule kwa kuwa hakuna kama wewe mwingine yaani wewe au mimi ni watofauti sana ukilinganisha na mwingine,na huo utofauti wetu ndio thamani yetu.Kile kitu kinachokutofautisha na mimi ndio kitu kinachoutambulisha ubora wako ,thamani yako, uwezo wako na yamkini upekee ulionao. Kila mtu duniani amepewa kitu cha kufany

KIPIMO UNACHOPIMIA WENGINE NDICHO UTAKACHOPIMIWA

Habari zenu wanamafanikio ? Ni dhahiri kuwa MUNGU anatupenda sana kiasi kwamba ametupa tena nafasi kafika mwaka mwingine tena kuendelea kujifunza kutoka kwake kupitia watu mbalimbali kwa manufaa ya maisha yetu! Kipimo ni kiasi au kiwango Fulani chenye kizio kwa namna ya kifizikia lakini kwa namna kusudiwa hapa kipimo kinamaana ya kiwango cha matendo au mambo unayoyafanya kwa wengine ambayo yanaweza  kuwasaidia au yasiwasaidie kwa kutotosheleza kile walitaraji! Kuna namna umekuwa na uwezo wa kuwasaidia wengine kwa kiwango Fulani tuchukulie labda ni kilo kumi za mchele lakini wewe umetoa kilo tano usitegemee ukihitaji wewe utapewa kilo kumi la sivyo hukuwa na uwezo wa kutoa kilo kumi ndipo ukatoa tano. Upo wakati umekuwa ukilalamika kwa habari ya kutaka msaada Fulani kwa mtu Fulani uliyemuamini atafanya kwa kiwango Fulani ridhishi kwako na hakufanya hivyo, nataka nikuambie kabla hujaanza kulaumu na kulalamika kwamba mtu uliyemuamini na kumkubali namna hiyo angeweza kukutendea hivyo, u

NINAWEZA

Ndugu mpenzi msomaji na mfuatiliaji wa makala zetu tunakusalimu kwa kabila lako,bila shaka haujambo na unaendelea na mapambano kwa nguvu mpya na kasi zaidi ukifanya kazi kwa bidii ili kufikia kilele cha safari yetu. Karibu tena tuendelee kujifunza pamoja,Leo nataka tujifunze tabia ya kujiambia ninaweza... Sema ninaweza ! Ndio mimi naweza, Na ninataka akili yangu ifahamu hivyo kwamba ninaweza kwa hiyo akili yangu pia inaweza kufikiri zaidi ya kawaida juu ya utatuzi wa jambo kubwa/ tatizo ambalo kwa hali ya kawaida haliwezekani lakini ile kwamba hujaiwekea akili mipaka inatamani kuthibitisha kwamba hakika unaweza na ikifikiri zaidi kuna suluhu. Nataka mwili wangu utambue mimi ninaweza kufanya mambo makubwa zaidi ya vile unavyodhani na ulivyozoea kuvifanya hivyo linapotokea jambo kubwa linalohitaji nguvu zaidi, kabla ya kuwaza maumivu mwili utambue unaweza kufanya kwa kuangalia matunda ya jambo hilo badala ya maumivu ya muda mfupi tu. Natamani pia moyo wangu ukubali hakika ya k