USIOGOPE

Habari za wakati huu mpenzi msomaji na mfuatiliaji wa makala zetu. Ninayo imani kuwa uko vizuri kiafya na unaendelea kupambana. Karibu tushirikishane jambo hili.

Kama kipo Kitu MUNGU anathamini kwenye maisha ya kwako basi ni ule mpango yuko nao juu yako.
Kuna watu ambao umewaamini sana,ni watu wa karibu,mke au mume, wazazi,mpenzi, ndugu ,marafiki zetu tumewashirikisha kuhusu maisha yetu na mipango tuliyonayo na yamkini tukadhani tungepata kusaidika na badala yake, tumepata matokeo kinyume na taraja letu. Natamani nikutie moyo kwamba kama suala la mipango ya MUNGU kwetu lingekuwa la kawaida kwake basi isingekuwa rahisi,

Yusufu kuweza kuwa waziri mkuu na hatimaye ndugu zake kuwa chini yake kama MUNGU alivyokuwa amemuonesha kwenye maono kupitia njozi zake. Kwa sababu alipowashirikisha ndugu zake walikuwa tayari hata kumuua ili kile MUNGU amekusudia kwa Yusufu kisitokee.

Ayubu pia asingeweza kushinda jaribu alilopitia hususan ni pale ambapo mkewe anamshawishi amkufuru MUNGU ili afe, ndipo ujiulize Huyo mke alikuwa anaelewa maana ya usaidizi ama la? Je kweli alilijua kusudi la MUNGU kupewa Ayubu kama mumewe? Maana haikumsumbua kabisa kusema akufuru afe, akifa halafu?

Kwa mantiki hiyo kumbe rafiki, ndugu mpenzi, mke, mume hata wazazi wakwako wanaweza kuwa kikwazo kuzifikia ndoto zako. Kumbe watu ambao kwa kiwango kikubwa wanaweza kuyaathiri maisha yako ni wale wakaribu nawe na unaowaamini, japo wapo wazuri ambao wanaweza kukusaidia kuyafikia yale MUNGU amekusudia kwenye maisha yako,

mfano Daudi na Jonathan walikuwa marafiki siku hizi wanasema marafiki wa faida Kitu ambacho kilimtia moyo Daudi kwa habari ya wito wa kifalme, haikuwa rahisi lakini Rafiki aliposimama kwenye nafasi yake mambo yote yakawa sawa,

Ningesema angalia sana marafiki unaowachagua tena uchague wale unaodhani wanamsaada juu ya kile ulichokibeba lakini vipi kuhusu wazazi, ndugu pamoja na mkeo au mumeo? hao nao utawachagua tena? Si rahisi, sasa basi utambue kuwa Hakuna MTU wa kubatilisha mpango wa MUNGU kwenye maisha yako labda aamue yeye au wewe uruhusu iwe hivyo.

Usiogope unapokutana na hali yoyote ya kukukatisha tamaa kutoka kwa watu wa karibu kwa sababu wewe si wakwanza kutendwa nao isipokuwa unachopaswa kuangalia ni MUNGU aliyekupa hiyo zawadi aamue kwako na sio wanadamu, Usivunjike moyo MUNGU atalilinda kusudi hilo hadi litimie kuwa Mwaminifu. Yeye MUNGU aliyemwambia Mussa kwamba hata kama hajui kuongea ama anakigugumizi ni lazima atoke na Wanaisrael Misri kwenda Kaanani, Hata akamwambia Jeremia nalikujua tangu kabla misingi ya Dunia kuwepo,
hulitazama neno lake apate kulitimiza ,hatokuacha Usiogope!

.

Imeandikwa na Antony Mwakilima.
Mawasiliano:     0756 351 462
                             0672 314 874
email:     mwaijox@gmail.com      

       TAFAKARI BADILI MTAZAMO
                         ©2017

Comments

Popular posts from this blog

AVUMILIAYE MPAKA MWISHO NDIYE ATAKAYEOKOKA!

KIPIMO UNACHOPIMIA WENGINE NDICHO UTAKACHOPIMIWA

HASIRA HASARA