KIPIMO UNACHOPIMIA WENGINE NDICHO UTAKACHOPIMIWA

Habari zenu wanamafanikio ? Ni dhahiri kuwa MUNGU anatupenda sana kiasi kwamba ametupa tena nafasi kafika mwaka mwingine tena kuendelea kujifunza kutoka kwake kupitia watu mbalimbali kwa manufaa ya maisha yetu!

Kipimo ni kiasi au kiwango Fulani chenye kizio kwa namna ya kifizikia lakini kwa namna kusudiwa hapa kipimo kinamaana ya kiwango cha matendo au mambo unayoyafanya kwa wengine ambayo yanaweza  kuwasaidia au yasiwasaidie kwa kutotosheleza kile walitaraji!

Kuna namna umekuwa na uwezo wa kuwasaidia wengine kwa kiwango Fulani tuchukulie labda ni kilo kumi za mchele lakini wewe umetoa kilo tano usitegemee ukihitaji wewe utapewa kilo kumi la sivyo hukuwa na uwezo wa kutoa kilo kumi ndipo ukatoa tano.

Upo wakati umekuwa ukilalamika kwa habari ya kutaka msaada Fulani kwa mtu Fulani uliyemuamini atafanya kwa kiwango Fulani ridhishi kwako na hakufanya hivyo, nataka nikuambie kabla hujaanza kulaumu na kulalamika kwamba mtu uliyemuamini na kumkubali namna hiyo angeweza kukutendea hivyo, unapaswa ujiulize,ni wangapi ambao wamekuja kwako nawe ukawatendea sawasawa? Kumbuka vema je,yule aliyekuja kwako kukuomba elfu moja nawe ulikuwa na uwezo wa elfu tano lakini ukampa mia mbili hatoshi kukufanya wewe upimiwe kipimo hicho?

Yawezekana uliona ni jambo dogo ambalo haliwezi kumfanya mtu akulipizie kisasi au akutendee ubaya, kwa sababu ulilitenda wewe na aliumia mwingine hukuona ukubwa jambo hilo japo ulijua so jema, sasa basi kabla hujaanza kuhisi umeonewa , kabla hujaanza kuona haujatendewa haki ebu kaa utafakari hakuna yeyote kwenye maisha yako ulimtenda kama ulivyotendewa? Wakati mwingine unapotendewa huwezi kukumbuka Kirahisi kwa sababu siye uliyemtendea,

Lakini pia kuna wakati unashangaa unapokea msaada wakati ulikuwa huoni wakukusaidia kabisa na kwamba ukahisi hata ukiomba usaidiwe haitokuwa rahisi
Lakini unapata msaada kwa kiwango kidhi na ridhishi kabisa kana kwamba hauelewi imekuwaje! Lakini ukirejea nyuma kifkra unagundua kumbe ulishawahi kumtendea mtu mmoja vema ,ulimsaidia alipohitaji msaada wako kwa kiwango kikubwa chenye kumridhisha na kukidhi haja aliyokuwa nayo.

Unapaswa utambue kila unachokifanya kwa wengine kina madhara kwako pia na madhara hayo yaweza kuwa hasi au chanya. Ipo siku hayo yatafanyika kwako hata kama sio kwa kupitia wale uliowatendea wewe na kwa sababu hukumbuki kwa kuwa madhara yake yaliwapata uliowatendea.

pia inawezekana umekuwa huoni ukipiga hatua licha ya bidii unazofanya kumbe kuna watu hukuwatendea vema kwenye maisha yao na yale malalamiko yao vinyongo vyao vimekuwa vikidai haki yao na kufunga mafanikio yako bila ya kujua kipimo unapowapimia wengine utapimia nawewe kwa kipimo hichohicho unabakia kulalamika tu badala ya kutafakari kwa kina uone kama yupo uliyemtendea vibaya useme naye akuachilie(akusamehe) ili yeye awapo na amani nawe ndipo ufanikiwe, unaendelea kulaumu tu.

Kumbuka kutenda mema ni hazina huwezi kufanikiwa kwa kuwatendea ubaya wengine au kuombea mabaya yawapate wengine kwenye maisha yao. Jifunze kuwapimia wengine vipimo vizuri na vikubwa ili nawewe uje upimiwe vivyo hivyo. Utakavyo kutendewa watendee wengine. Usitarajie kuona watu wanakutendea unavyotaka utendewe kama wewe huwatendei wengine.

Kufanikiwa ni kipimo cha kuwafanya wengine wafanikiwe pale wanapokwama...je ni wangapi wamefanikiwa kupitia wewe?

   
Imeandikwa na Antony Mwakilima.
Mawasiliano:     0756 351 462
                             0672 314 874
email:     mwaijox@gmail.com      

       TAFAKARI BADILI MTAZAMO
                         ©2017

Comments

Popular posts from this blog

AVUMILIAYE MPAKA MWISHO NDIYE ATAKAYEOKOKA!

HASIRA HASARA