KAZA MKANDA VIZURI

Habari za Leo mpenzi na mfuatiliaji wa makala za blog yetu! Ni matumaini yangu u bukheri wa afya njema. Ningependa nikukaribishe kwa mara nyingine tujifunze zaidi, kwa ajili ya kuendelea kupiga hatua mbele zaidi. Mungu awe pamoja nawe karibu!

Kaza mkanda vizuri
Najua kuna wakati umekuwa ukisafiri kondakta akakwambia funga mkanda. Ni kweli ni vizuri kufunga mkanda uwapo safarini hata kama hukai siti za nyuma ya gari lakini kufunga mkanda kunasaidia kupunguza mitikisiko na mishituko inayoweza kujitokeza aidha gari ikipitishwa kwenye bamzi unakuwa salama ,na Mimi nasisitiza usifunge tu hakikisha unakaza kabisa mkanda bila kujali uko siti gani. Si kwa manufaa yangu wala kondakta Ila ni kwa faida yako mwenyewe.

Ninahakika umezoea kuona mikanda ikifungwa hasa kwenye suruali zenye viuno vikubwa kuliko cha mvaaji. Leo nataka nikwambie hata kama suruali yako unahisi haihitaji mkanda kwa kuwa imekukaa vizuri nakuambiaje funga mkanda na ukaze vizuri, hakuna anayejua badae kutatokea nini hivyo usipofunga mkanda mtu anaweza kuivuta ikaanguka ukaadhirika. Haijalishi ni kubwa, saizi ya kati au ni ndogo hakikisha unafunga mkanda na kukaza vizuri iyo suruali yako.
Ninamaanisha sisi watu tunatofautiana sana mitazamo yetu ambayo inatutofautishia suruali zetu(maono, ndoto, malengo, matazamio) kuna wenye malengo ya kawaida, madogo na makubwa! Kipimo cha ukubwa au udogo hutegemea na ulinganishi.

Unajilinganisha na nani ili useme maono yako ni makubwa, ya kati au madogo. Bila kujali ni madogo au makubwa nakusihi funga mkanda kama huna mkanda tumia hata kamba usiweke visingizio ikaze vizuri maana mwenye nacho ataongezewa naye asiyenacho hata kidogo alichonacho atanyang'nywa, usisubiri ianguke ndipo uifunge uzuri itakugharimu ,weka juhudi usimtegemee mtu kwamba ukikwama atakuinua, Unachokiona wewe niwewe pekee utakayeweza kukichukua mfano wanafunzi wa Yesu wangeliona kama Yesu alivyoona wasingeshindwa kuomba hata saa moja.

Hakuna atakayeweza kubeba aibu yako suruali ikikuanguka ni lazima ujue hilo, ndoto zako zikikwama hakuna atayejishughurisha nazo hata kama alikuunga mkono awali,ukishindwa kufunga mkanda wewe ukaachia ilegee uwe na hakika ipo siku utataka kuipandisha ukute ishaanguka.
Kama bado hujaanza kufunga mkanda au kamba anza sasa bila kuchelewa! Wewe ndiye uwezaye kushika na kumiliki unachokiona ukisubiri ushikiwe watakushikia cha kwao na usigundue ukawa mtumwa wao!
        FUMBUA MACHO ONGEZA UPEO.

Imeandikwa na Antony Mwakilima.
Mawasiliano:     0756 351 462
                             0672 314 874
email:     mwaijox@gmail.com      

       TAFAKARI BADILI MTAZAMO
                         ©2017

Comments

Popular posts from this blog

AVUMILIAYE MPAKA MWISHO NDIYE ATAKAYEOKOKA!

KIPIMO UNACHOPIMIA WENGINE NDICHO UTAKACHOPIMIWA

HASIRA HASARA