NINAWEZA

Ndugu mpenzi msomaji na mfuatiliaji wa makala zetu tunakusalimu kwa kabila lako,bila shaka haujambo na unaendelea na mapambano kwa nguvu mpya na kasi zaidi ukifanya kazi kwa bidii ili kufikia kilele cha safari yetu.
Karibu tena tuendelee kujifunza pamoja,Leo nataka tujifunze tabia ya kujiambia ninaweza...

Sema ninaweza!
Ndio mimi naweza,
Na ninataka akili yangu ifahamu hivyo kwamba ninaweza kwa hiyo akili yangu pia inaweza kufikiri zaidi ya kawaida juu ya utatuzi wa jambo kubwa/ tatizo ambalo kwa hali ya kawaida haliwezekani lakini ile kwamba hujaiwekea akili mipaka inatamani kuthibitisha kwamba hakika unaweza na ikifikiri zaidi kuna suluhu.

Nataka mwili wangu utambue mimi ninaweza kufanya mambo makubwa zaidi ya vile unavyodhani na ulivyozoea kuvifanya hivyo linapotokea jambo kubwa linalohitaji nguvu zaidi, kabla ya kuwaza maumivu mwili utambue unaweza kufanya kwa kuangalia matunda ya jambo hilo badala ya maumivu ya muda mfupi tu.

Natamani pia moyo wangu ukubali hakika ya kwamba ninaweza na usizimie kwa ugumu wala uzito wa mambo yanayoendelea au yatakayojitokeza kwa sababu ninaweza hivyo nao unaweza kustahimili mambo makubwa ya maumivu au namna yoyote ambayo unaweza ukasita kuyachukulia na kusamehe, ninaweza!.

Kama akili ,moyo na mwili vimekubali ninaweza basi ni dhahiri kwamba macho nayo hayatataka kuuangusha mwili yataanza kuona mbali zaidi ya viwango vya kawaida, masikio vilevile yatajifunza kusikiliza na kuzingatia zaidi, hata nitakapoituma mikono haitakuwa na uvivu wa kushika na kufanya vizuri zaidi pia miguu haitaogopa umbali tena kwa sababu ninaweza.
Kwa nini niseme naweza? Ninataka mwili,akili na moyo viwe tayari kujaribu mambo mengi zaidi bila kujali ugumu wala uzito wake nipate nguvu ya kuthubutu. Naam moyo useme ninaweza kubeba changamoto zote pasipo kuchoka nayo Akili iseme sitachoka kufikiri maana ninaweza kuleta ufumbuzi. Lakini mwili nao useme sitajali maumivu wala uchovu wowote maana ninaweza kustahimili ugumu na maumivu pasipo kuchoka mpaka nione matokeo mazuri ninayotarajia.

Jiambie sasa unaweza naam usiruhusu mashaka wala kusita kwa sababu ni kweli unaweza, sema ninaweza kwa kuwa tunayaweza yote kwake yeye atutiaye nguvu!

Imeandikwa na Antony Mwakilima.
Mawasiliano:     0756 351 462
                             0672 314 874
email:     mwaijox@gmail.com      

       TAFAKARI BADILI MTAZAMO
                         ©2017

Comments

Popular posts from this blog

AVUMILIAYE MPAKA MWISHO NDIYE ATAKAYEOKOKA!

KIPIMO UNACHOPIMIA WENGINE NDICHO UTAKACHOPIMIWA

HASIRA HASARA