MAHUSIANO.
weza kuwa kikwazo kikubwa cha maendeleo.
MUNGU mwenyewe alianzisha mahusiano kwa kumpenda mwanadamu hata kumuumba kwa mfano wake na alipopotoka bado alimuokoa kupitia Yesu Kristo Mnazareti.
Chanzo cha mahusiano kwa upande wa wanadamu ni Adamu na Hawa. Mwanaume ni mtu ambaye aliaminiwa na MUNGU akapewa maelekezo kamili na halisi kuhusu maisha ya edeni. Majukumu yalikuwa mengi nae MUNGU akaona ni vema amtafutie msaidizi na hapa ndipo inabidi tujifunze kuona tofauti ya upendo wa kweli na vinginevyo. Adamu alifanyiwa viumbe vingi ambavyo vililetwa kuwa Msaidizi wake hakupenda kusaidiwa navyo (huwa kuna swali linanisumbua hapa kwamba, ni kazi gani aliyokuwa nayo Adamu ambayo ilimpasa kubagua na kuchagua msaidizi bora zaidi kuliko wote aliofanyiwa na MUNGU?) Tuachane na hilo swali sio mpango wangu kwa sasa tuangalie hatima ya uchaguzi wa Adamu ilikuwa ni Eva. Sasa suala la kuliangalia hapa ni baada ya Eva kupatikana ambaye alitokana na nyama na mifupa yake naye akamkubali kuwa msaidizi wake.
Swali je, ni kweli Adamu alimpa maelekezo(Instructions) Eva kama ilivyompasa?
Hebu tuone, Tangu Adamu alipoumbwa Hatujaona pahali ambapo shetani akizururazurura Edeni, kwa nini? Unajua shetani anatambua fika Adamu amepokea maelekezo moja kwa moja kutoka kwa MUNGU mwenyewe, hivyo alikuwa anaujua uzito wa maelekezo hayo. Ni kama fasihi simulizi ilivyo hupoteza sifa na ubora inapotoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mtu mwingine. Nataka kusema yamkini Adamu hakumpa Eva maelekezo kamilifu na yenye msisitizo kama ambavyo alikuwa amepewa yeye ndio sababu kubwa shetani hakumfuata Adamu na badala yake alimfuata Eva na kumdanganya kwa kuwa alitambua uzito wa maelekezo hayo Adamu hakuisisitiza kwa Eva.
Upendo ulishazaliwa kati ya Adamu na Eva lakini shida inayotokea hapa ni 'maelekezo' naye shetani hutumia sana upenyo huu kwa watu wengi katika mahusiano hata kuwagombanisha na MUNGU. Adamu alimpenda kweli Eva ndio maana alimtii Eva baada ya kudanganywa na joka hata kula tunda lililokatazwa. Hapa ndipo unapoona suala la udhaifu wa Mwanaume ni mwanamke linapozaliwa. Mwanaume anapaswa kumpenda mwanamke kiasi cha kuona udhaifu wake ni huyo mwanamke ampendaye kwamba anaweza kufanya mambo magumu ili kumlinda na kuonesha anamjali.
Wapi tunakosea sasa?
Makosa makubwa tunayoyafanya wanaume wengi ni kujisahau kutoa maelekezo kamili kuhusu kile anachopaswa kusaidiwa na Eva kwa sababu Eva haji na kitu kipya anakuja na nguvu/uwezo (strength) tu ambao anapaswa atumie kukusaidia Adamu kuyatimiza maelekezo uliyobeba kwa hiyo kama hukumpa maelekezo kamili yamkini akakusaidia kulingana na maelekezo yako.
Unapokuwa kwenye mahusiano wewe unatoa maelekezo kamili? Maelekezo yampasayo? Au unatoa nusunusu ?
Ukiona umempa maelekezo pungufu Eva wako uwe na uhakika shetani yupo karibu kuja kumpa maelekezo ambayo pengine yasipingane sana na yale uliyompa ila yakamfanya amuamini shetani na kufanya alichoelekezwa nae hivyo kuwatenganisha ninyi kwa ninyi na kuwatenganisha na MUNGU, na hicho ndicho kilichotokea kwa Adamu na Eva edeni!
Man should not fail to provide Godly instructions to his woman as well as woman should obey such instructions for only this can improve relationships all the way.
Kwa nini?
Kwa sababu MUNGU alitengana na mwanadamu kwa kukosa utii kwenye maelekezo aliyoyatoa.
Uhusiano wa wengi wetu unavunjika kwa kukosa maelekezo sahihi na pia hata yakipatikana hakuna utii.
Wanaume na watoe maelekezo kamili nao wanawake watii maelekezo hayo. Naongelea maelekezo ya kimungu kwa maana kile umeitwa ufanye na vile ungependa mwanamke wako awe kulingana na vile mnapaswa kuishi chini ya maelekezo hayo. Kana kwamba udhaifu wa mwanaume uwe ni mwanamke ampendae nayo nguvu ya mwanamke iwe ni mwanaume ampendae.
Hii ndio sababu wengi tunatupiana lawama Mara mwanamke Mara mwanaume lakini kila mmoja akitenda kwa nafasi yake hakuna wakulaumiwa. MUNGU atusaidie tuweze kutenda itupasavyo.
Imeandikwa na Antony Mwakilima.
Mawasiliano: 0756 351 462
0672 314 874
email: mwaijox@gmail.com
TAFAKARI BADILI MTAZAMO
©2017
Comments
Post a Comment