Posts

Showing posts from March, 2017

KIONDOE HICHO KIUNGO

Natamani kuzungumza na mtu mmoja saa hii. Habari yako ndugu, jamaa na rafiki yangu? Naamini u mzima wa afya njema na unaendelea kukaza buti ukifanya juhudi kufikia mafanikio ya ndoto zako. Karibu tena ndugu, leo tatazungumzia habari ya kuondoa au kung'oa au kutoa kiungo kwamishi. Kiungo kinacholeta vikwazo kwa safari tuliyonayo ya mafanikio. Kuna Kitu ambacho usipokijua kitakusumbua sana kitakufanya wakati mwingine uishi maisha ya utumwa na unapokuja kushituka unakuta tayari mambo yamekwisha haribika na huna tena muda wa kuishi maisha yakwako. Imeandikwa ukiona kiungo chochote cha mwili wako kinakukosesha king'oe, kiondoe au kitoe kisiwe sehemu yako kwa sababu ni heri ukose kiungo kimoja uende uzimani kuliko kuwa na viungo vyote jehanamu. Ni kitu gani basi kitakachokupa wewe maumivu makubwa namna hii zaidi ya mwili wako? Kama ni hivyo mbona unataka kufanikiwa lakini umeendelea kukumbatia marafiki wanaokukwamisha? Hao marafiki ulionao mbona hawakusaidii kuishi maisha uliyo

CONNECTION

Habri rafiki zangu? Nafurahi kwa sababu natambua tuko pamoja na tunaendelea kunufaika na vitu ambavyo Mungu hutufundisha juu ya maisha yetu ili tuweze kusonga mbele hata kufikia yale maisha ameyakusudia kwetu. Karibu tena tushirikishane kuhusu Connection. Napenda kusema neno kidogo kuhusu connection(muunganiko au uhusiano), unajua watu wote tunapenda mambo mazuri yatokee kwenye maisha yetu. Kuna wakati tumekutana na fursa mbalimbali tumeshindwa kwa sababu tunapenda mambo mazuri tu bila connection. Napozungumzia connection namaanisha uhusiano kati ya hicho unachokipenda na upatikanaji wake. Nitakupa mfano wengi wetu tumezoea kutumia maneno yafuatayo, ninayaweza yote kwake yeye anitiaye nguvu... Amesema tutashinda na zaidi ya kuahinda, atatufanya kichwa na si mkia n.k zipo nukuu nyingi tu ambazo tumekuwa tukitembea nazo. Sasa nataka ujiulize tangu umeanza kutembea na hizi nukuu umeona tofauti? kwanini unashindwa? Kwanini huwi kichwa? Ukiwa mwanafunzi hakuna Kitu kinatiliwa mkazo uwap

HADITHI YA KUKU

Habari ya leo rafiki yangu, siku yako imekaaje? Natumaini tuko pamoja na tunaendelea kujifunza pamoja karibu tena tujifunze kupitia kisa cha kuku. Jifunze kutoka kwa kuku .... Ninayo hadithi fupi ya kweli ambayo imetokana na kitu nilichojifunza kwa kuku mmoja nikiwa ninalima shamba. Unajua unapotambua kuwa kuku na wao wanakula ndipo unapojua kuwa nawao wanatafuta ulaji(ridhiki)! Sasa basi kulikuwa na kuku watatu wawili matemba na mmoja jogoo. Miongoni mwa matemba alikuepo temba mmoja mdogo, huyu ndiye aliyenisukuma nikuhadithie habari hizi. Huyu kuku alikuwa anatafuta chakula chake na haikuwa tu chakula lakini ni wadudu ambao huwa ni adamu kipindi cha kiangazi na mbaya zaidi wanaishi ndani ya ardhi. Ni wadudu fulani jamii ya funza weupe wanapendwa sana na kuku! Mambo niliyoyaona kwa kuku huyo, 1 ) Huyu kuku alijua anachokiataka . Licha ya kuzungukwa na kuku wengine wakubwa bado hakuwa muoga, hakuwaogopa kuku wenzie cha ajabu kabisa hata mimi na jembe hakutuogopa alichokiangal

UNAPOKUWA MWANAMKE!

Habari ya wakati huu wapendwa wasomaji wa makala zetu. Nikupe hongera kwa kuendelea kuweka muda wako kwa ajili yetu ili tujifunze pamoja. Karibu tusherehekee kwa namna hii siku hii ya leo ambapo mama zetu,wapenzi wetu,rafiki zetu wa kike na ndugu zetu wanaadhimisha siku yao. Unayonafasi kubwa sana Duniani,kuna vitu vingi sana vinanisukuma kusema hivi mfano pasipo mwanamke isingekuwa rahisi Yesu kuja duniani kama mwanadamu,haijalishi mimba ilitungwaje tunachojua alikuja duniani kupitia mwanamke,sijui ni wanawake wangapi wanaiona hii nafasi kubwa kabisa waliyopewa na MUNGU,kulibeba kusudi kubwa la wokovu wa wengi.Upande mwingine Mwanamke ndiye mtunza familia ndiye anayejua nani yuko wapi anafanya nini wakati gani,Kitu ambacho mwanaume huelezwa tu kama taarifa anaejua kipi kimepungua kipi kinahitajika nyumbani, hela si tatizo, tatizo ni Jana tulikula hiki na Leo tule kile husimamia yeye.Anategemewa na familia, amefanywa kuwa msaidizi wa mwanaume yaani uwepo wake ni kumfanya mwanaume aw

ANGALIA USIVYOVIONA

Angalia Usivyoviona ! Habari rafiki zangu? Ninayofuraha kuwashirikisha kuhusu kuangalia usivyoviona. Unaweza kujiuliza utawezaje kuangalia usivyoviona. Kuangalia si lazima vionekane unapoamua kuangalia maana yake unaanza kuzingatia ni tofauti kidogo na kutazama ambapo ni lazima uone kile unachokitazama. Suala la kuangalia visivyoonekana ni suala ambalo humfanya mtu aanze kuona kwamba ili awe asivyoviona anahitaji kuwa tofauti. Nini maana visivyoonekana? Unajua maisha yako ya kesho ni Kitu ambacho hukioni, hizo ndoto ulizonazo za kutaka kuwa mtu mkubwa sana baadae ni Kitu usichokiona, hiyo mipango ya kumiliki jumba na magari ya kutembelea bado havionekani, unapoifikilia mbingu na uzima wa milele unapata picha ya vitu visivyoonekana,unaambiwa kuhusu imani ni lazima uanze kufikiria visivyoonekana, ukifuatilia vizuri vitu vingi usivyoviona ni vizuri mno, vinavutia, vinapendeza na kutia hamasa pia. Kama unatazamia kuwa mfanyabiashara mkubwa, msanii maarufu au mtu fulani mwenye hadhi ku