Posts

Showing posts from 2016

USIMDHARAU MTU YEYOTE

Habari yako mpenzi msomaji wetu?Bila shaka u mzima wa afya.Ni wakati mwingine tena siku nyingine tukiwa na hamasa nyingine nakukaribisha tuungane pamoja kujifunza juu ya usimdharau MTU yeyote! USIMDHARAU MTU Ndio natumaini kila mmoja wetu kama binadamu yawezekana kabisa kuna mazingira umekutana nayo kwenye maisha ukawadharau wengine au kuna Hadhi umepata ikakupelekea uone wewe pekee ndio unamaana na umuhimu.Nataka nikuambie usimdharau mtu awayeyote kwa sababu, Bado hujajua kila Kitu Yawezekana kwa hilo ulifanyalo wapo wenye maarifa zaidi ukiwadharau hutayapata.usijione kwamba huwezi tena kuhitaji maarifa yoyote kutoka kwa wengine, ni muhimu sana kujua hili ikiwa unataka kufanikiwa ni lazima uwe mchezaji mzuri wa timu yako ,maarifa yetu yanatofautiana na uwezo wa kufanya mambo vilevile kwa hiyo badala ya kudharauliana,golikipa anapaswa asimdharau mfungaji wake ama beki ili waweze kushirikiana vizuri hebu tushikane mikono kama timu tucheze pamoja ndivyo wengine wanavyofunga mago

HASIRA HASARA

Image
Habari za leo rafiki yangu!bila shaka uko vizuri na unapiga hatua kila unaporuhusu ubongo wako upokee vitu vipya na kukuongezea thamani katika maisha yako. Leo ni siku nyingine tena tunayofuraha kuungana pamoja kujifunza kuhusu hasira hasara ,hebu jiulize ni mara ngapi umeruhusu hasira iamue juu ya hatima ya maisha yako licha ya kuijua methali hii? unadhani maamuzi uliyochukua ukiwa na hasira yamekuwa chanya kwenye maisha yako? kama hasira imekupa athari hasi za maamuzi uliyochukua ukiwa umeudhiwa ,umechukua hatua gani hata sasa? Naomba upate muda utafakari kiasi ambacho maisha yako yameathiriwa kutokana na maamuzi uliyofanya ukiwa na hasira, hebu mtazame Kaini alichofanya baada ya kutawaliwa na hasira alimuua nduguye Abeli, na baada ya hapo akaingia kwenye laana ambayo hakika ilisababisha maisha yake yasiende vizuri. Yawezekana kabisa alijua kwamba akiua ndugu yake mambo yake yatakuwa mazuri na pengine atakubalika badala yake kampoteza ndugu na laana juu. Je,ni mara ngapi umesikia

AVUMILIAYE MPAKA MWISHO NDIYE ATAKAYEOKOKA!

Habari ya uzima mpenzi msomaji wa makala zetu,tunayofuraha kuzidi kuendelea kujifunza pamoja nawe.Siku ya leo ni siku ya pekee kabisa ambayo tunakwenda kuzungumzia habari ya kuvumilia mpaka mwisho. Kuvumilia ni kule kukabiliana na changamoto zozote unazokutana nazo pasi na kukata tamaa,kurudi nyumba au kukubali kushindwa. Anayevumilia ni yule asiyekuwa tayari kushindwa licha ya ugumu anaoupitia. Kuvumilia kuna ukomo tofauti tofauti kulingana na mtu binafsi na ugumu husika anaoupitia. Kwa uzito uleule wa kazi fulani au changamoto fulani,wapo watu wa makundi yafuatayo kuhusiana na viwango vya uvumilivu wao. WANAOVUMILIA MUDA MFUPI TU. Kuna wengine huweza kuvumilia changamoto kwa muda mfupi tu na kukata tamaa au kuchoka kabisa na asiwe tayari kuendelea tena. Hawa wengi wao wanakuwa bado hawajayakaribia mafanikio kabisa yaani wanapothubutu tu kufanya jambo la kuwapeleka kwenye mafanikio, wakikutana na changamoto hukimbia kana kwamba wanapokimbilia hakuna changamoto. Hawa wanadhani

SIKU YA FURAHA NI LEO

Ninayofuraha siku nyingine tena kushirikiana ujumbe huu pamoja nawe mpenzi msomaji wa makala katika blog yetu,sina shaka unaafya njema na unaendelea kuweka bidii kwa ajili ya kuifikia safari ya mafanikio tuyatakayo! Ndio siku ya furaha ni leo! Tunapaswa kuiishi leo kana kwamba ni siku ya mwisho,tukiishi kwa furaha! Lazima usahau kuhusu jana ndipo unaweza kuishi leo vizuri na kwa furaha kwa sababu, Jana imekuwa ni siku ya kuumiza kwako,umeumizwa kwa mambo mengi mfano mahusiano, dhuluma, magonjwa, kuonewa, kushindwa na kukatishwa tamaa, kukataliwa n.k Jana imekuwa ni siku ya huzuni sana kwako,umehuzunishwa na misiba ya watu waliokuwa msaada wako wa karibu, unafiki wa marafiki na wale uliowaamini, ugumu wa maisha, utawala wa rushwa n.k Jana imekuwa ni siku ilijaza moyo wako uchungu kutokana na mateso ya mama wa kambo, ndugu wenye roho mbaya, kuibiwa na kunyang'anywa haki, kunyanyasika kutokana na hali ya umaskini,kupanda kwa gharama za maisha n.k Kuna wakati kutokana na jana iki

THAMANI UNAYOTOA SI SAWA NA WANAYOIPOKEA

Image
Ninayofuraha kukualika tena rafiki mpendwa mfuatiliaji wa makala zetu,ni imani yangu kuwa wewe ni mzima wa afya kabisa na unaendelea vizuri katika yote unayojishughurisha nayo kuhahakikisha unafikia mafanikio yale uyatakayo. Ni siku nzuri tena ninayotaka tushirikishane juu ya unavyotoa kwa wengine na namna ambavyo wanavipokea na ukubwa ambao wanavichukulia vile unavyovitoa. Ni mara nyingi sana watu wengi wamekuwa wanashindwa kutoa kwa sababu wanadhani kwamba kila anayepewa anahitaji kikubwa ili aitambue thamani ya mtoaji. Nimekuwa shahidi wa jambo hili ndio maana nimeamua nikushirikishe ili tupate ufahamu huu wa ajabu ,mimi nimejifunza kwamba inapofikia hatua ya kumfanyia mtu kitu watu wengi tumekuwa na kasumba ya kujithaminisha kwa kuangalia kazi au shughuri unazofanya na jinsi ambavyo mtu huyo unayetaka kutoa kwake mnaheshimiana kiasi gani? au atakuchukuliaje ukitoa kwake hicho unachotaka kutoa? Yawezekana umefikia hatua hii kwa sababu unadhani unachotaka kutoa ni kidogo sana na

FANYA UNACHOKIPENDA

Habari ya leo tena mpendwa msomaji na rafiki yangu ?ni matumaini yangu kuwa uko na afya njema kabisa inayoimarika kila siku kwa ajili ya kukuwezesha kuweka bidii zaidi hata kufikia mafanikio uyatakayo. Ni vema sana kuupa mwili wako kile unataka kwa ajili ya kuwa na afya njema ,nguvu na kukupa ujasiri wa kupambana mpaka umeona mafanikio au umepata kile unachotaka. Fanya unachopenda mwenyewe. Nasisitiza tena fanya unachokipenda wewe mwenyewe.Hapa nazungumzia habari ya kufanya chochote halali chenye matokeo chanya kwenye maisha yako na yanayokuzunguka,kuna mambo mengi mazuri unatamani kuyafanya kutoka moyoni mwako lakini pengine umekutana na wanaokupinga usifanye au wanaokuzuia kufanya hicho kisichoharamu unachopenda kufanya. kwa nini ufanye unachokipenda? Kufanya unachokipenda itakufanya 1/uweke bidii kubwa tofauti na yule anayefanya kitu asichokipenda au anayeshinikizwa kufanya jambo asilolipenda. Ndio wengi wameshindwa kutimiza ndoto zao au maono yao ya kimaisha kutokana na kufan

ATHARI HASI KUTOKANA NA WATU WAKO WA KARIBU

Image
Natumaini kuwa hujambo na unaendelea vizuri na mapambano ya maisha kuhakikisha unapata unachotaka. Nashukuru Mungu ni siku nyingine njema ambayo tunaendelea kujifunza juu ya mambo ambayo hutusaidia kufikia vilele vya mafanikio tunayoyataka.                        Ndio kuna athari nyingi hasi ambazo zimetokana na ndugu zetu,rafiki zetu,wapenzi wetu ,wazazi wetu pia ambazo zimechangia kuwa na maisha tuliyonayo sasa aidha kwa ushawishi wao kwako juu ya kile wanachokiamini au kwa shinikizo kutoka kwao ufanye kipendacho roho zao. Wapo ambao wamekushurutisha au kukulazimisha na kukushinikiza kufanya jambo ambalo moyo wako haukuwa tayari wala wewe binafsi hukulipenda lakini kwa heshima yao ukafanya ili waridhike bila kujua kwamba kufanya kitu usichopenda ambapo unakuwa hauko tayari, hauna amani na hufurahii kufanya kunapunguza ufanisi, ubunifu na ueledi wako kwa jambo ulipendalo. Kuna watu wameolewa kwa kulazimisha aidha kutokana na umasikini au tamaa za wazazi wao,wengine wameachana na we

ACHA KUTAMANI KUWA KAMA MWINGINE.

Habari ya wasaa huu rafiki zangu naimani nyote hamjambo na mnaendelea kuyafanyia kazi tunayojifunza kila wakati,nataka tujifunze kuhusu saikolojia ya kutammani kuwa kama mtu fulani au mtu mwingine,saikolojia hii ni kwamba hutafanya cha kwako ila cha yule unaetamani kuwa kama yeye. Ndio ni muhimu sana kulitambua hili usitamani kuwa kama mimi na mimi nisitamani kuwa kama wewe kwa sababu ifuatayo ,kama mimi nikitamani kuwa kama wewe ,je ni nani atakayefanya kile Mungu amekusudia kifanyike kupitia mimi?pia kama wewe ukitamani kuwa kama mimi nani basi atakayefanya kile ambacho Mungu ametaka kifanyike duniani kupitia wewe?.Hii ndio sababu muhimu ya kukwambia usitake kuwa kama yeyote yule kwa kuwa hakuna kama wewe mwingine yaani wewe au mimi ni watofauti sana ukilinganisha na mwingine,na huo utoafauti wetu ndio thamani yetu.Kile kitu kinachokutofautisha na mimi ndio kitu kinachoutambulisha ubora wako ,thamani yako, uwezo wako na yamkini upekee ulionao. Kila mtu duniani amepewa kitu cha kufa

USIPUUZE HALI YOYOTE ISIYO YA KAWAIDA KIAFYA INAPO KUTOKEA

Ndio ni siku nyingine tena na wasaa mwingine MUNGU ametupatia nafasi ya kukutana katika blog yetu hii nzuri inayokuelimisha kwa habari za afya lakini tukilenga zaidi mafanikio.nikushukuru kwa kufanya uamuzi wa busara kwa kujipa muda huu wathamani sana kujifunza nasi kupitia makala hii nikukaribishe rasmi tuendelee na mada yetu. Ni kweli usipuuze inamaana sana kuutambua mwili wako unapokuwa na afya njema ili iwe rahisi kujua mambo yanapobadilika kiafya katika mwili wako afya inapoyumba .utajiuliza maswali mengi kwamba ni kwa nini nakuambia usipuuze,ni kwamba .... (A)kila hali isiyoyakawaida katika mwili wako inauwezo wa kuathiri utendaji wako wa kila siku.kutokana na udhaifu au unyonge wa mwili kuna mambo hautayafanya kwa viwango vinavyotakiwa japo utakuwa unajiona uko sawa kumbe sivyo.hali hiyo inaweza kukufanya ukawa mvivu kufanya kazi na kuathiri uzalishaji wako.Ndio ukiathiri uzalishaji unawaathiri wahitaji hivyo kama ni mkulima unamuathiri mfanyabiashara ambaye atahama kwako kwen

DAWA YA MADONDA YA TUMBO

Je unasumbuliwa na madonda ya tumbo na hujui utafanyaje   ili kuyatibu fuatana na mimi kwenye Makala hii.                                                    Fuata hatua zifuatazo kuandaa dawa Andaa Jani moja la Alovera safisha vizuri. Lichane katikati kisha liloweke kwenye maji kiasi kwa muda wa nusu saa . Chukua(majani ya madasa ni maarufu kwa watu wa kanda ya ziwa au majani ya matatila kwa watu wa nyanda za juu kusini )haya ni majani   ambayo yana sifa ya kushika nguo na hupatikana shambani- tumia robo   tatu ya majani hayo kisha safisha kuondoa vumbi subiri kidogo maji ulosafishia yakauke. Kisha twanga hayo majani kwenye kinu . Chukua lita moja na nusu ya maji kisha changanya na majani uliyoyatwanga. Tikisa vizuri mchanganyiko wako ukishachanganya uzuri . Chukua maji ya jani la alovera(alojuicy) uliyochuja yachanganye na mchanganyiko wako wa madasa . Hakikisha unatikisa vizuri mchanganyiko wako ili alovera na madasa vichanganyike vizuri katika lita moja na nusu ya maji .