Posts

Showing posts from 2017

A LIVING DOG IS BETTER THAN A DEAD LION

How are you doing? Hope you are all just fine. Its my hope everything is going as planned. I invite you once again to learn together about importance of being alive. There are lots of staffs happen to our lives because we do not give life that value of it. Imagine if car engine dies. Can any movement be made? Can starter work as usual? no more movement can be made using that car. If a plant dies, we don't expect of getting any healthier food from it. What does this mean? Actually it is obvious to see people busy struggling for their ongoing when alive. We know, all strong, rich and great people we ever knew after their death no more stories about. Everything concerns their fame goes off memory. The history perishes, and the things get changed. If you go check the family left by thee, you will wonder to see them in so different and hard life otherwise you will find them in conflicts every one wants to be part of the legacy. Very few families remain stable and probably their coo...

UKITAKA CHUMA KUWA SUMAKU

Habari yako mpendwa mfuatiliaji wa makala zetu za mafanikio,afya na tabia. Tunajua ili tufanikiwe kwenye yale tunayoyafanya tunahitaji watu ambao tutaendana nao kitabia, kiufanisi na kiuadilifu. Nakukaribisha tena siku ya leo tujifunze kutoka kwa sumaku. Kuna watu wanajiuliza nitamjuaje wa kufanana naye? Ninayeendana naye? Najua kuna mtu unamtafuta ufanye naye kitu mfano biashara, kuna mtu unamtafuta ujenge naye urafiki, uchumba n.k Yaani kuna sifa unatamani mtu Fulani awe nazo ndipo uweze kufanya naye jambo fulani kama mifano tajwa hapo juu. Nataka nikueleze, ukimkuta kichaa jaani hushangai, lakini mtu aliyetimamu ukimkuta huko bila shaka lazima ushangae. Ndio kuna mazingira ambayo huwezi kuwakuta nzi wako wengi kama mazingira machafu. Kuna watu unataka ushirikiane nao katika jambo kwenye maisha yako wakiwa na sifa fulani lakini unashindwa kuwajua. Iko wazi kwamba ndege wanaofanana ndio wanaoruka pamoja, swali ni je,utamjuaje binadamu unayefanana naye katika hilo unalotaka kulifan...

MAHUSIANO.

weza kuwa kikwazo kikubwa cha maendeleo. MUNGU mwenyewe alianzisha mahusiano kwa kumpenda mwanadamu hata kumuumba kwa mfano wake na alipopotoka bado alimuokoa kupitia Yesu Kristo Mnazareti. Chanzo cha mahusiano kwa upande wa wanadamu ni Adamu na Hawa. Mwanaume ni mtu ambaye aliaminiwa na MUNGU akapewa maelekezo kamili na halisi kuhusu maisha ya edeni. Majukumu yalikuwa mengi nae MUNGU akaona ni vema amtafutie msaidizi na hapa ndipo inabidi tujifunze kuona tofauti ya upendo wa kweli na vinginevyo. Adamu alifanyiwa viumbe vingi ambavyo vililetwa kuwa Msaidizi wake hakupenda kusaidiwa navyo (huwa kuna swali linanisumbua hapa kwamba, ni kazi gani aliyokuwa nayo Adamu ambayo ilimpasa kubagua na kuchagua msaidizi bora zaidi kuliko wote aliofanyiwa na MUNGU?) Tuachane na hilo swali sio mpango wangu kwa sasa tuangalie hatima ya uchaguzi wa Adamu ilikuwa ni Eva. Sasa suala la kuliangalia hapa ni baada ya Eva kupatikana ambaye alitokana na nyama na mifupa yake naye akamkubali kuwa msaidizi wak...

KIONDOE HICHO KIUNGO

Natamani kuzungumza na mtu mmoja saa hii. Habari yako ndugu, jamaa na rafiki yangu? Naamini u mzima wa afya njema na unaendelea kukaza buti ukifanya juhudi kufikia mafanikio ya ndoto zako. Karibu tena ndugu, leo tatazungumzia habari ya kuondoa au kung'oa au kutoa kiungo kwamishi. Kiungo kinacholeta vikwazo kwa safari tuliyonayo ya mafanikio. Kuna Kitu ambacho usipokijua kitakusumbua sana kitakufanya wakati mwingine uishi maisha ya utumwa na unapokuja kushituka unakuta tayari mambo yamekwisha haribika na huna tena muda wa kuishi maisha yakwako. Imeandikwa ukiona kiungo chochote cha mwili wako kinakukosesha king'oe, kiondoe au kitoe kisiwe sehemu yako kwa sababu ni heri ukose kiungo kimoja uende uzimani kuliko kuwa na viungo vyote jehanamu. Ni kitu gani basi kitakachokupa wewe maumivu makubwa namna hii zaidi ya mwili wako? Kama ni hivyo mbona unataka kufanikiwa lakini umeendelea kukumbatia marafiki wanaokukwamisha? Hao marafiki ulionao mbona hawakusaidii kuishi maisha uliyo...

CONNECTION

Habri rafiki zangu? Nafurahi kwa sababu natambua tuko pamoja na tunaendelea kunufaika na vitu ambavyo Mungu hutufundisha juu ya maisha yetu ili tuweze kusonga mbele hata kufikia yale maisha ameyakusudia kwetu. Karibu tena tushirikishane kuhusu Connection. Napenda kusema neno kidogo kuhusu connection(muunganiko au uhusiano), unajua watu wote tunapenda mambo mazuri yatokee kwenye maisha yetu. Kuna wakati tumekutana na fursa mbalimbali tumeshindwa kwa sababu tunapenda mambo mazuri tu bila connection. Napozungumzia connection namaanisha uhusiano kati ya hicho unachokipenda na upatikanaji wake. Nitakupa mfano wengi wetu tumezoea kutumia maneno yafuatayo, ninayaweza yote kwake yeye anitiaye nguvu... Amesema tutashinda na zaidi ya kuahinda, atatufanya kichwa na si mkia n.k zipo nukuu nyingi tu ambazo tumekuwa tukitembea nazo. Sasa nataka ujiulize tangu umeanza kutembea na hizi nukuu umeona tofauti? kwanini unashindwa? Kwanini huwi kichwa? Ukiwa mwanafunzi hakuna Kitu kinatiliwa mkazo uwap...

HADITHI YA KUKU

Habari ya leo rafiki yangu, siku yako imekaaje? Natumaini tuko pamoja na tunaendelea kujifunza pamoja karibu tena tujifunze kupitia kisa cha kuku. Jifunze kutoka kwa kuku .... Ninayo hadithi fupi ya kweli ambayo imetokana na kitu nilichojifunza kwa kuku mmoja nikiwa ninalima shamba. Unajua unapotambua kuwa kuku na wao wanakula ndipo unapojua kuwa nawao wanatafuta ulaji(ridhiki)! Sasa basi kulikuwa na kuku watatu wawili matemba na mmoja jogoo. Miongoni mwa matemba alikuepo temba mmoja mdogo, huyu ndiye aliyenisukuma nikuhadithie habari hizi. Huyu kuku alikuwa anatafuta chakula chake na haikuwa tu chakula lakini ni wadudu ambao huwa ni adamu kipindi cha kiangazi na mbaya zaidi wanaishi ndani ya ardhi. Ni wadudu fulani jamii ya funza weupe wanapendwa sana na kuku! Mambo niliyoyaona kwa kuku huyo, 1 ) Huyu kuku alijua anachokiataka . Licha ya kuzungukwa na kuku wengine wakubwa bado hakuwa muoga, hakuwaogopa kuku wenzie cha ajabu kabisa hata mimi na jembe hakutuogopa alichokiangal...

UNAPOKUWA MWANAMKE!

Habari ya wakati huu wapendwa wasomaji wa makala zetu. Nikupe hongera kwa kuendelea kuweka muda wako kwa ajili yetu ili tujifunze pamoja. Karibu tusherehekee kwa namna hii siku hii ya leo ambapo mama zetu,wapenzi wetu,rafiki zetu wa kike na ndugu zetu wanaadhimisha siku yao. Unayonafasi kubwa sana Duniani,kuna vitu vingi sana vinanisukuma kusema hivi mfano pasipo mwanamke isingekuwa rahisi Yesu kuja duniani kama mwanadamu,haijalishi mimba ilitungwaje tunachojua alikuja duniani kupitia mwanamke,sijui ni wanawake wangapi wanaiona hii nafasi kubwa kabisa waliyopewa na MUNGU,kulibeba kusudi kubwa la wokovu wa wengi.Upande mwingine Mwanamke ndiye mtunza familia ndiye anayejua nani yuko wapi anafanya nini wakati gani,Kitu ambacho mwanaume huelezwa tu kama taarifa anaejua kipi kimepungua kipi kinahitajika nyumbani, hela si tatizo, tatizo ni Jana tulikula hiki na Leo tule kile husimamia yeye.Anategemewa na familia, amefanywa kuwa msaidizi wa mwanaume yaani uwepo wake ni kumfanya mwanaume aw...

ANGALIA USIVYOVIONA

Angalia Usivyoviona ! Habari rafiki zangu? Ninayofuraha kuwashirikisha kuhusu kuangalia usivyoviona. Unaweza kujiuliza utawezaje kuangalia usivyoviona. Kuangalia si lazima vionekane unapoamua kuangalia maana yake unaanza kuzingatia ni tofauti kidogo na kutazama ambapo ni lazima uone kile unachokitazama. Suala la kuangalia visivyoonekana ni suala ambalo humfanya mtu aanze kuona kwamba ili awe asivyoviona anahitaji kuwa tofauti. Nini maana visivyoonekana? Unajua maisha yako ya kesho ni Kitu ambacho hukioni, hizo ndoto ulizonazo za kutaka kuwa mtu mkubwa sana baadae ni Kitu usichokiona, hiyo mipango ya kumiliki jumba na magari ya kutembelea bado havionekani, unapoifikilia mbingu na uzima wa milele unapata picha ya vitu visivyoonekana,unaambiwa kuhusu imani ni lazima uanze kufikiria visivyoonekana, ukifuatilia vizuri vitu vingi usivyoviona ni vizuri mno, vinavutia, vinapendeza na kutia hamasa pia. Kama unatazamia kuwa mfanyabiashara mkubwa, msanii maarufu au mtu fulani mwenye hadhi ku...

KAZA MKANDA VIZURI

Habari za Leo mpenzi na mfuatiliaji wa makala za blog yetu! Ni matumaini yangu u bukheri wa afya njema. Ningependa nikukaribishe kwa mara nyingine tujifunze zaidi, kwa ajili ya kuendelea kupiga hatua mbele zaidi. Mungu awe pamoja nawe karibu! Kaza mkanda vizuri Najua kuna wakati umekuwa ukisafiri kondakta akakwambia funga mkanda. Ni kweli ni vizuri kufunga mkanda uwapo safarini hata kama hukai siti za nyuma ya gari lakini kufunga mkanda kunasaidia kupunguza mitikisiko na mishituko inayoweza kujitokeza aidha gari ikipitishwa kwenye bamzi unakuwa salama ,na Mimi nasisitiza usifunge tu hakikisha unakaza kabisa mkanda bila kujali uko siti gani . Si kwa manufaa yangu wala kondakta Ila ni kwa faida yako mwenyewe. Ninahakika umezoea kuona mikanda ikifungwa hasa kwenye suruali zenye viuno vikubwa kuliko cha mvaaji. Leo nataka nikwambie hata kama suruali yako unahisi haihitaji mkanda kwa kuwa imekukaa vizuri nakuambiaje funga mkanda na ukaze vizuri, hakuna anayejua badae kutatokea nini hiv...

USIOGOPE

Habari za wakati huu mpenzi msomaji na mfuatiliaji wa makala zetu. Ninayo imani kuwa uko vizuri kiafya na unaendelea kupambana. Karibu tushirikishane jambo hili. Kama kipo Kitu MUNGU anathamini kwenye maisha ya kwako basi ni ule mpango yuko nao juu yako. Kuna watu ambao umewaamini sana,ni watu wa karibu,mke au mume, wazazi,mpenzi, ndugu ,marafiki zetu tumewashirikisha kuhusu maisha yetu na mipango tuliyonayo na yamkini tukadhani tungepata kusaidika na badala yake, tumepata matokeo kinyume na taraja letu. Natamani nikutie moyo kwamba kama suala la mipango ya MUNGU kwetu lingekuwa la kawaida kwake basi isingekuwa rahisi, Yusufu kuweza kuwa waziri mkuu na hatimaye ndugu zake kuwa chini yake kama MUNGU alivyokuwa amemuonesha kwenye maono kupitia njozi zake. Kwa sababu alipowashirikisha ndugu zake walikuwa tayari hata kumuua ili kile MUNGU amekusudia kwa Yusufu kisitokee. Ayubu pia asingeweza kushinda jaribu alilopitia hususan ni pale ambapo mkewe anamshawishi amkufuru MUNGU ili afe, n...

ACHA KUTAMANI KUWA KAMA MWINGINE.

Habari ya wasaa huu rafiki zangu naimani nyote hamjambo na mnaendelea kuyafanyia kazi tunayojifunza kila wakati,nataka tujifunze kuhusu saikolojia ya kutamani kuwa kama mtu fulani au mtu mwingine,saikolojia hii ni kwamba hutafanya cha kwako ila cha yule unaetamani kuwa kama yeye. Ndio ni muhimu sana kulitambua hili usitamani kuwa kama mimi na mimi nisitamani kuwa kama wewe kwa sababu ifuatayo ,kama mimi nikitamani kuwa kama wewe ,je ni nani atakayefanya kile Mungu amekusudia kifanyike kupitia mimi?pia kama wewe ukitamani kuwa kama mimi nani basi atakayefanya kile ambacho Mungu ametaka kifanyike duniani kupitia wewe?.Hii ndio sababu muhimu ya kukwambia usitake kuwa kama yeyote yule kwa kuwa hakuna kama wewe mwingine yaani wewe au mimi ni watofauti sana ukilinganisha na mwingine,na huo utofauti wetu ndio thamani yetu.Kile kitu kinachokutofautisha na mimi ndio kitu kinachoutambulisha ubora wako ,thamani yako, uwezo wako na yamkini upekee ulionao. Kila mtu duniani amepewa kitu cha kufany...

KIPIMO UNACHOPIMIA WENGINE NDICHO UTAKACHOPIMIWA

Habari zenu wanamafanikio ? Ni dhahiri kuwa MUNGU anatupenda sana kiasi kwamba ametupa tena nafasi kafika mwaka mwingine tena kuendelea kujifunza kutoka kwake kupitia watu mbalimbali kwa manufaa ya maisha yetu! Kipimo ni kiasi au kiwango Fulani chenye kizio kwa namna ya kifizikia lakini kwa namna kusudiwa hapa kipimo kinamaana ya kiwango cha matendo au mambo unayoyafanya kwa wengine ambayo yanaweza  kuwasaidia au yasiwasaidie kwa kutotosheleza kile walitaraji! Kuna namna umekuwa na uwezo wa kuwasaidia wengine kwa kiwango Fulani tuchukulie labda ni kilo kumi za mchele lakini wewe umetoa kilo tano usitegemee ukihitaji wewe utapewa kilo kumi la sivyo hukuwa na uwezo wa kutoa kilo kumi ndipo ukatoa tano. Upo wakati umekuwa ukilalamika kwa habari ya kutaka msaada Fulani kwa mtu Fulani uliyemuamini atafanya kwa kiwango Fulani ridhishi kwako na hakufanya hivyo, nataka nikuambie kabla hujaanza kulaumu na kulalamika kwamba mtu uliyemuamini na kumkubali namna hiyo angeweza kukutendea hivy...

NINAWEZA

Ndugu mpenzi msomaji na mfuatiliaji wa makala zetu tunakusalimu kwa kabila lako,bila shaka haujambo na unaendelea na mapambano kwa nguvu mpya na kasi zaidi ukifanya kazi kwa bidii ili kufikia kilele cha safari yetu. Karibu tena tuendelee kujifunza pamoja,Leo nataka tujifunze tabia ya kujiambia ninaweza... Sema ninaweza ! Ndio mimi naweza, Na ninataka akili yangu ifahamu hivyo kwamba ninaweza kwa hiyo akili yangu pia inaweza kufikiri zaidi ya kawaida juu ya utatuzi wa jambo kubwa/ tatizo ambalo kwa hali ya kawaida haliwezekani lakini ile kwamba hujaiwekea akili mipaka inatamani kuthibitisha kwamba hakika unaweza na ikifikiri zaidi kuna suluhu. Nataka mwili wangu utambue mimi ninaweza kufanya mambo makubwa zaidi ya vile unavyodhani na ulivyozoea kuvifanya hivyo linapotokea jambo kubwa linalohitaji nguvu zaidi, kabla ya kuwaza maumivu mwili utambue unaweza kufanya kwa kuangalia matunda ya jambo hilo badala ya maumivu ya muda mfupi tu. Natamani pia moyo wangu ukubali hakika ya k...

USIANGALIE ULIONAO ANGALIA WATAKAOKUJA

Habari ya siku ya leo mpendwa msomaji wa makala mbalimbali katika blog yetu?ni matumaini yangu kuwa uko vizuri na unaendelea kupambana kuhakikisha unakuwa na maisha unayoyataka lakini kwa ajili ya wengine yaani watu wa kundi lako. Karibu tena tuendelee kuongeza thamani kwenye maisha yetu. Haijalishi ulikuwa na kundi LA watu au marafiki kiasi gani kwenye maisha yako Jana. Maamuzi yako yatakayoibadilisha kwanza Leo na kuleta kesho mpya yanayo matokeo mawili. (1) Yanaweza kupelekea kuongezeka kwa marafiki wapya au idadi ya watu wa kundi lako . Hili likitokea wengi hatuna mashaka wala hatuogopi na tunaona ni kawaida na maisha yanaendelea. Yamkini iko hivi kwa sababu bado unaeleweka yaani hujabadilika umeendelea kuwa yuleyule kila siku hata ukiamua kubadilika unabadilika kidogo sana bila kuathiri maisha ya hilo kundi ulilonalo na pia inawezekana ukaona kawaida kwa sababu kila siku marafiki huongezeka, inabidi utambue sio kawaida ukiona kundi lako linaongezeka ujue unahitaji nguvu zaidi...

UNAVYOTOA SI SAWA NA WANAVYOPOKEA

Ninayofuraha kukualika tena rafiki mpendwa mfuatiliaji wa makala zetu,ni imani yangu kuwa wewe ni mzima wa afya kabisa na unaendelea vizuri katika yote unayojishughurisha nayo kuhahakikisha unafikia mafanikio yale uyatakayo. Ni siku nzuri tena ninayotaka tushirikishane juu ya unavyotoa kwa wengine na namna ambavyo wanavipokea na ukubwa ambao wanavichukulia vile unavyovitoa. Ni mara nyingi sana watu wengi wamekuwa wanashindwa kutoa kwa sababu wanadhani kwamba kila anayepewa anahitaji kikubwa ili aitambue thamani ya mtoaji. Nimekuwa shahidi wa jambo hili ndio maana nimeamua nikushirikishe ili tupate ufahamu huu wa ajabu ,mimi nimejifunza kwamba inapofikia hatua ya kumfanyia mtu kitu watu wengi tumekuwa na kasumba ya kujithaminisha kwa kuangalia kazi au shughuri unazofanya na jinsi ambavyo mtu huyo unayetaka kutoa kwake mnaheshimiana kiasi gani? au atakuchukuliaje ukitoa kwake hicho unachotaka kutoa? Yawezekana umefikia hatua hii kwa sababu unadhani unachotaka kutoa ni kidogo sana na k...

USIACHE KUWA MTOTO KWA WAZAZI WAKO

Ahsante sana mpenzi msomaji kwa kuendelea kujifunza pamoja nasi yale yanayotuwezesha kuwa na maisha bora yenye furaha kila iitwapo leo, sina shaka u mzima wa afya kabisa. Naomba nikukaribishe kwenye mada ya leo ambayo tunakwenda kujifunza habari ya kuendelea kuwa mtoto kwa wazazi wako , kusema hivi haina maana ya kuendelea kudeka kwa wazazi wako,kuendelea kuwategemea kwa kila unachokihitaji au kuendelea kuwapa mzigo wa kukulea ungali mtu mzima ambaye unayomajukumu na unauwezo wa kujitegemea kimaisha bali namaanisha kwamba kuna hatua za kimaisha watu wakifikia husahau kabisa kuwa wao ni watoto kwa wazazi wao na kwamba haijalishi wana nafasi gani kwenye jamii yao wataendelea kuwa watoto kwa wazazi wao. Kuna mambo mengi yamepelekea watu wakasahau kuwa wanapofika kwa wazazi wao wanaendelea kuwa watoto na pia inawapasa waendelee kuwaheshimu na kuwanyenyekea hata kuwa msaada kwao kwa kubeba jukumu la malezi pale wanapokuwa hawawezi tena yaani wamezeeka au hawana nguvu tena za kuwasaidia ...